Top Ad unit 728 × 90

Inspector Haroun a.k.a 'BABU' Moja ya majembe niliyokuwa nayakubali sana na nimeyamis kitambo sana katika game la kibongo Hii hapa ni stori kwa ufupi toka alipoanzia muziki miaka ile ya nyuma


Haroun Kahena (maarufu kama Inspector Haroun) ni mwanamuziki kutoka Temeke, Dar es Salaam, nchini Tanzania. Yuko katika kundi la Tmk Wanaume Halisi. Inspector Haroun ni Mtoto wa Mzee Kahena aishiye huko Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam.

Maisha ya Muziki

Haroun alianza kazi muziki mnamo miaka ya 1990 na amefanya kazi kadhaa kipindi cha nyuma na wanamuziki wengine tofauti kabla ya kujiunga na Tmk Wanaume Halisi. Alitoa nyimbo ya kwanza mwaka 1998, 'Mauzauza', akiwa na Luteni Karama kwenye kundi la Gangwe Mobb. Baada ya hapo wakatoa nyingine mwaka 2000 'Mtu Be,' kisha wakatoa Wimbo wa 'Mtoto wa Geti Kali' ulimpatia umaarufu mkubwa. Aliutoa wimbo huu peke yake ingawa alikuwa bado yupo katika kundi la Gangwe Mobb.

Miaka ya Hivi karibuni kulitokea na kutokuelewana na mwenzake Luteni Kalama hali iliyosababisha kuvunjika kwa kundi la Gangwe Mobb japo kuna taarifa kwamba kundi hili limerudi tena kama zamani hapo bado hawajatoa kazi za kutosha za kulifanya kundi liwe 'HOT' kama ilivokuwa miaka ya nyuma

Albamu Alizotoa Akiwa Gangwe Mobb

  • Simulizi La Ufasaha (2001)
  • Nje Ndani (2002)
 
Hapa BABU akiwa na Lady Jay Dee 'Komando'
Inspector Haroun a.k.a 'BABU' Moja ya majembe niliyokuwa nayakubali sana na nimeyamis kitambo sana katika game la kibongo Hii hapa ni stori kwa ufupi toka alipoanzia muziki miaka ile ya nyuma Reviewed by Unknown on Wednesday, July 18, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.