Top Ad unit 728 × 90

MUSIC 28 PRODUCTIONS Kutana na Producer MSWAKI MABITI


Music 28 ni studio mpya jijini na itakayofunguliwa siku za hivi karibuni kwa lengo moja tu la kuja kuteka na ku-run Music Industry nchini Tanzania. Studio hii iko chini ya Producer Mahiri na Professional (Young Talented Producer) Mswaki Mabiti kama anavyojulikana na wengi.

Mswaki ni Producer Pia ni Msanii wa Bongo Fleva ambaye alishatoa ngoma zake kadhaa ikiwa ni track za kwake mwenyewe pamoja na track alizokwisha watolea wasanii mbalimbali wa Bongo akiwemo Beka msanii kutoka THT na Ditto pia kutoka THT na wimbo wake unaowika sana hadi sasa ‘TUSHUKURU KWA YOTE’ na wimbo wa Q Chilla ambao upo juu sana kwa hivi sasa ‘UNGENIUMIZA.

Kazi zake mwenyewe ambazo alishawahi kufanya ni nyimbo iliyomtambulisha katika Ramani ya Muziki wa Bongo Fleva ulioitwa ‘Hasira’ ambao aliutengeneza yeye mwenyewe ndani ya Jazz Record enzi hizo akishirikiana na Producer Q pamoja na Tuddi ambaye kwa sasa yupo Ngoma Rec.

Alishafanya kazi na wasanii mbalimbali akiwemo Linah, Linex, Izzo Business, Slim Sal, Nuruel, Nikki wa Pili pamoja na wengine wengi ambao kashirikiana nao na pia kawatengenezea ngoma akiwa Producer na vili vile alishapitia studio kadhaa jijini ikiwemo Dreams record pamoja na Jazz Rec na hivi sasa ndo yupo katika hatua za mwisho kukamilisha Studio na Rec Lebo yake ya MUSIC 28.

Producer Mswaki Mabiti toka Music 28
  Wenye vipaji wote mnakaribishwa toka pande zote za nchi kwa ajili ya kufanya kazi na MSWAKI.. 
Download hapa Beat ya Hasira yake Mswaki nawe ukachanie mamistari
MUSIC 28 PRODUCTIONS Kutana na Producer MSWAKI MABITI Reviewed by Unknown on Friday, July 20, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.