Top Ad unit 728 × 90

MWENGE WA UHURU LEO KULALA MVUMI MISSION

Mwenge wa Uhuru
Mbio za mwenge wa Uhuru zinaendelea nchini na sasa upo mkoani Dodoma ambapo ushazungua maeneo mbalimbali na leo hii unatarajia kulala pale Mvumi Mission  ambapo kutakuwa na mambo mbalimbali yatakayokuwa yakiendelea eneo lile ukiachana na huo mkesha.

Kutatolewa burudani mbalimbali kama ninavofahamu lazima kutakuwa na Muziki pamoja na Sinema zitakazokuwa zikiendelea.

Ila Angalizo langu kwa Vijana na watu wa Rika zote wenyeji na kwa wageni wote nikimaanisha watakaokuwa wapo katika mbio hizo za mwenge ni kwamba tujiheshimu na kujitambua sisi wenyewe hasa ukizingatia mikesha kama hii vijana wengi na hata watu wazima wenye familia zao wanatumia muda huu kufanya mambo ambayo yapo kinyume na maadili hasa katika upande wa Ngono na Anasa Vijana ndo wanaona muda muafaka.

Ngoma ya Asili (Cigogo)
 
Tafadhali ukiwa kama kijana na mwenye kujitambua tumia muda huu kujifunza vitu na sio kuutumia mkesha huu kujipunguzia maisha au kujitafutia makovu yasiyofutika katika maisha yako.

UKIMWI UNAUA – kasha kwa maendeleo ya eneo lako na sio kukesha kwa ngono na wake za watu

MWENGE WA UHURU LEO KULALA MVUMI MISSION Reviewed by Unknown on Saturday, July 21, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.