MFAHAMU RAPA NA MCHEZA SINEMA MKONGWE QUEEN LATIFAH
Dana Elaine
Owens (amezaliwa tar. 18 Machi,
1970), anafahamika zaidi
kwa jina lake la kisanii kama Queen Latifah, ni rapa, mwigizaji,
na mwimbaji
kutoka nchini Marekani.
Kazi zake Queen Latifah katika muziki, filamu na televisheni zimepelekea kupata
tuzo ya Golden Globe, Screen Actors Guild Awards mbili, Image Awards mbili, Grammy Award,
amechaguliwa mara sita kwenye Grammy, na kuchaguliwa tena kwenye Emmy Award
na Academy Award.
Queen Latifah |
Maisha ya awali
Latifah alizaliwa na kukulia mjini Newark,
New Jersey, binti wa Rita, mwalimu wa shule ambaye alifanya kazi katika
shule ya Irvington High School ya mjini New Jersey, na Lancelot Owens,
Sr, ambaye ni afisa wa polisi. Wazazi wake walitalikiana wakati Latifah akiwa na umri wa miaka kumi. Latifah alikulia katika kanisa la Kibaptist. Jina lake la kisanii, Latifah , maana yake "laini" na "mwanana" kwa Kiarabu,
alipewa jina hilo na binamu yake wakati ana umri wa miaka minane. Daima
msichana shupavu, urefu wa futi 5'10" wa Latifah alikuwa mtu wa mbele
katika timu ya mpira wa kikapu ya shuleni kwake. Aliimba kipengele cha "Home" kutoka katika filamu ya muziki ya The Wiz katika mchezo wa kuigiza wa shuleni kwake
Kazi za muziki
Mwanzo (1988–1989)
Latifah alianza beatboxing kwa ajili kundi la rap la Ladies Fresh.
Latifah alikuwa mmoja kati ya wanachama wa toleo halisi la Flavor Unit,
ambalo, kwa kipindi hicho, -likuwa kundi la Ma-MC walioungana na
mtayarishaji DJ Mark the 45 King.
Mnamo 1988, DJ Mark the 45 King alisikia toleo la mfano (demo) la
single ya Latifah "Princess of the Posse" na kutoa demo ile kwa Fab Five Freddy, ambaye alikuwa mtangazaji wa Yo! MTV Raps.
Kurap (1989–2002)
Freddy alimsaidia Latifah kuingia mkataba na Tommy Boy Records, ambao ndiyo waliotoa albamu ya kwanza ya Latifah, All Hail the Queen
mnamo 1989, akiwa na umri wa miaka kumi na tisa. Mwaka huo, alionekana
kama mwamuzi kwenye UK label Music of Life album "1989—The Hustlers
Convention (live)". Mnamo 1998, ashirikiana na Ro Smith sasa ni Afisa
Mtendaji Mkuu wa Def Ro Inc. akaweza kutayarisha na kutoa albamu yake ya
nne ya hip-hop, Order in the Court.
Kuimba (2003–2007)
Baada ya Order in the Court, Latifah akahamia jumla katika
uimbaji wa mashairi ya muziki wenye viwango vya soul na jazz, ambapo
awalia alikuwa akifanya kama ziada wakati anafanya rekodi za hip hop
hapo awali. Mnamo 2004, ametoa albamu ya soul/jazz The Dana Owens Album. Mnamo tar. 11 Julai, 2007, Latifah aliimba katika Hollywood Bowl
mjini Los Angeles ikiwa kama kifunguzi cha tamasha la moja kwa moja la
jazz. Kabla ya kundi la watu wanaizidi kiaisi cha 12,400, nyuma yake
kulikuwa na watu wanaopig vyombo wakiwa kumi na wengine watatu
waimbaji-wa-kwa-nyuma, huitwa The Queen Latifah Orchestra. Baadaye 2007,
Latifah ametoa albamu iliyoitwa Trav'lin' Light. Jill Scott, Erykah Badu, Joe Sample, George Duke, Christian McBride, na Stevie Wonder wameuza sura ndani yake. It was nominated for a Grammy in the "Best Traditional Pop Vocal Album" category.
Mnamo 2009, Latifah, akiwa pamoja na Jubilation Choir, wamerekodi kibao kwenye albamu ya Oh Happy Day: An All-Star Music Celebration, wameurudia wimbo wa Oh Happy Day wa kina Edwin Hawkins Singers waliopatia umaarufu mnamo 1969.
Kurudi katika hip hop (2008–mpaka sasa)
Mnamo 2008, Latifah aliulizwa kama anaweza kutengeneza albamu
nyingine ya hip hop. Alinukuliwa akisema kwamba albamu isha-kamilika
tayari na itaitwa "All Hail the Queen II". Kulikuwa na fununu ya kwamba
albamu ingeitwa "The 'L' Word". Alipoulizwa kuhusu fununu hizo, alieleza
kwamba lilikuwa jaribio lake tu la "kuvuruga mibichwa ya watu"
wanamzania kwamba ni msagaji. Mnamo tar. 12 Septemba, 2008, Rolling Stone waliitoa taarifa ya kwamba Queen Latifah anapika albamu yake mpya itakayoitwa Persona.
Kasha la albamu hii linafanana na mchezo wa videoo wa Shin Megami
Tensei: Persona. Wimbo "Cue the Rain" ulitolewa ukiwa kama single
kiongozi kutoka katika albamu. Pia kuna wimbo kaimba na Missy Elliott.
Filamu na televisheni
Kazi za awali (1993–2001)
Kuanzia 1993-1998, Latifah alikuwa na uhusika katika ucheshi wa Living Single uliokuwa ukirushwa na Fox,
pia alitunga na kuimba kwenye kibwagizo cha ucheshi huo. Alianza kazi
zake za uigizaji wa filamu kwenye uhusika-saidizi wa mnamo 1991 na 1992
kwenye filamu za House Party 2, Juice, na Jungle Fever. Alikuwa na kipindi chake mwenyewe cha majadiliano kilichokwenda kwa jina la The Queen Latifah Show, kuanzia mwaka wa 1999 mpaka 2001. Pia alipata kuwa na uhusika wa kurudia-rudia kwenye msimu wa pili (1991-1992) wa kipindi mashuhuri cha NBC, The Fresh Prince of Bel-Air. Amepata kucheza kama mgeni mwalikwa kwenye ucheshi wa Hangin' with Mr. Cooper mnamo 1993. Latifah ameonekana katika filamu kali ya mwaka wa 1996, Set It Off na kisha baadaye kupata uhusika-saidizi katika filamu ya Holly Hunter , Living Out Loud (1998). Amecheza kama Thelma mnamo 1999 kwenye filamu ya Jeffrey Deavers, The Bone Collector, akiwa sambamba na Denzel Washington na Angelina Jolie.
Mafanikio (2002–mpaka sasa)
Studio albums
- All Hail the Queen (1989)
- Nature of a Sista (1991)
- Black Reign (1993)
- Order in the Court (1998)
- The Dana Owens Album (2004)
- Trav'lin' Light (2007)
- Persona (2009)
MFAHAMU RAPA NA MCHEZA SINEMA MKONGWE QUEEN LATIFAH
Reviewed by Unknown
on
Thursday, July 19, 2012
Rating:
No comments: