PICHA MBALIMBALI ZA UOKOAJI WA MIILI YA WATU BAHARINI
Waokoaji wakiwa kazini kwenye Meli ya Kilimanjaro
Muokoaji akiwa na maiti
Waokoaji wakiwa na majeruhi kwenye moja ya Boti za uokoaji.
Majeruhi wa wakipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja
MV KMKM ikiwa kazini
Raia wa kigeni wakiwasili Bandarini baada ya kuokolewa
Majeruhi wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi
Kavu na Majini (SUMATRA) imesema, meli iliyozama jana katika kisiwa cha
Chumbe, Zanzibar ilikuwa na abiria 248 wakiwemo watoto 31.
Kwa mujibu wa Sumatra, meli hiyo,
inamilikiwa na Kampuni Seagul Transport, imasajiliwa na Mamlaka ya
Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) na kwamba, Cheti cha Ubora kimeanza
tarehe 24 Agosti, 2011 na kinamalizika 23 Agosti, 2012. Imesema, meli
hiyo ilikuwa imeruhusiwa kubeba abiria wanaoruhusiwa 300 na tani 26 za
mizigo.
SUMATRA kupitia Kituo cha Utafutaji na
Uokoaji (MRCC) ilipata taarifa kuwa meli ya MV Skagit iliyokuwa
safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar ilikuwa inazama katika
eneo la karibu na kisiwa cha Chumbe, Zanzibar, eneo ambalo lipo umbali
wa Kilomita za Bahari 13.8 kutoka Bandari ya Zanzibar.
Zoezi la uokoaji linaendelea katika
eneo la tukio kutoka kwa Mv Flying Horse, Mv Kilimanjaro III, Tug
Bandari ya Zanzibar, KMKM, Mv Zanzibar I, Police Patrol Boat, Navy.
Chanzo:www.francisgodwin.blogspot.com
PICHA MBALIMBALI ZA UOKOAJI WA MIILI YA WATU BAHARINI
Reviewed by Unknown
on
Thursday, July 19, 2012
Rating:
No comments: