ZIJUE AINA ZA HIP HOP YA PWANI YA MASHARIKI NA PWANI YA MAGHARIBI
East Coast hip hop
East Coast hip hop ni jina la fomu ya muziki wa hip hop ambao unaasili na kukuzwa mjini New York City, Marekani,
mwanzoni mwa miaka ya 1970 na 1980. Mtindo huu ulianza kujulikana hasa
baada ya wasanii wengine kutoka sehemu mbalimbali za Marekani na
kuongezea staili tofauti. East Coast hip hop ulifahamika sana kama ndiyo
fomu halisi ya muziki wa hip hop.
West Coast hip hop
West Coast hip hop ni jina la kutaja aina ya muziki wa hip hop ambao umewazunguka wasanii wowote au muziki wowote wa hip hop wenye chimbuko la kanda ya magharibi mwa nchi ya Marekani. Japokuwa utamaduni wa muziki wa hip hop ulipewa jina lake huko mjini New York City,
lakini bado huaminika na baadhi ya watu kwamba utamaduni ulijianzisha
wenyewe kwa pande zote mbili, yaani, East na West coasts, kwa mtiririko
sawa.
ZIJUE AINA ZA HIP HOP YA PWANI YA MASHARIKI NA PWANI YA MAGHARIBI
Reviewed by Unknown
on
Thursday, July 19, 2012
Rating:
No comments: