Top Ad unit 728 × 90

CHADEMA WAPIGWA MABOMU MKOANI MOROGORO

NYUZZZZZ!!!UPDATES ...

MMOJA AFARIKI, WAWILI WAJERUHIWA KATIKA VURUGU MJINI MOROGORO LEO

Mwili wa Alli Zolla aliyedaiwa kuuwa na polisi kwa kupigwa risasi kichwani wakati wa vurugu zilizotokea leo asubuhi katika stendi ya mabasi Msamvu ukiwa hospitali ya mkoa wa Morogoro.
Kijana Hashimu Seif aliyepigwa risasi mguuni akiwa hospitali.
Kijana Frank Valimba akionyesha majeraha aliyoyapata tumboni kutokana na vurugu…

MSIMAMO WANGU KUHUSU VURUGU, RISASI, KUJERUHI NA “KUUA” MOROGORO - JOHN MNYIKA

 Baadhi ya vijana waliokuwa kwenye maandamano wakikamatwa na polisi mjini Moro leo.
Niliwahi kutahadharisha baada ya tukio la Dkt Stephen Ulimboka kuwa serikali imeanza kutumia mbinu haramu kudhibiti fikra mbadala, CCM imeanza kuongoza serikali kiimla na ipo siku umma utafikia hatua ya kukiona kama chama cha mauaji. Raia watatu wasio na hatia wamefyatuliwa risasi na mmoja amefariki. Haya yamefanyika kwenye maandamano ya amani ya wananchi kuwapokea viongozi wa CHADEMA kuelekea kwenye mkutano. Vurugu zimeanzishwa na polisi kwa mujibu wa mashuhuda wa ushahidi wa video. Vyanzo vyangu vinaniambia sasa wameagiza gari tatu za FFU na gari za kuwasha toka Dar Es Salaam. Tuombe MUNGU wasiamue kuvuruga mkutano wa hadhara ambao wananchi wamekusanyika kwa wingi hivi sasa maisha ya wachache yako mashakani lakini si mabadiliko kwa maslahi ya wengi.
John Mnyika.
27/08/2012.


Tanzama matukio ya picha.







CHADEMA WAPIGWA MABOMU MKOANI MOROGORO Reviewed by Unknown on Monday, August 27, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.