Top Ad unit 728 × 90

‘IZZO B’ KUACHIA VIDEO YA ‘UTARUDISHWA’ IJUMAA IJAYO…!!

MSANII wa muziki wa kizazi kipya anayewakilisha mkoa wa Mbeya Izzo B, amesema kuwa Ijumaa hii inayokuja video ya ngoma yake ya ‘Utarudishwa’ itakuwa sokoni katika muonekano mpya ambao haujawahi kutokea katika video nyingi za wasanii wa kibongo.

Pia Izzo aliweza kusema kwamba video hiyo imeshakamilika na kinachosubiriwa ni kuitoa ili mashabiki waweze kuona kilichofanyika.

Izoo alisema kuwa anaamini kazi yake iko poa hivyo hana wasiwasi sokoni kwani kila kazi anayotoa inakubalika ingawa wimbi la wasanii linampa changamoto ya kufanya kazi nzuri ambayo itaendelea kumpa heshima kutokana na jina lake.

“Video yangu inakuja nadhani Ijumaa hii inayokuja hivyo mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwani kitu kimetulia, kama wanavyojua mara zote huwa nafanya kazi ambazo mashabiki wangu wakisikiliza wanapata mzuka kutokana na mashairi na hata mtiririko wa ngoma njisi ulivyopangwa,” alisema.

‘IZZO B’ KUACHIA VIDEO YA ‘UTARUDISHWA’ IJUMAA IJAYO…!! Reviewed by Unknown on Sunday, September 23, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.