Top Ad unit 728 × 90

Abdukiba, Ali kiba kupamba 'Dunia Mapito'

Alisema kwa sasa yupo kwenye hatua za mwisho za uandaaji wa kazi hiyo, na anaamini kwamba itafanya vizuri kutokana na uwepo wa kaka yake.
Mbali na hilo aliweza kuwataka mashabiki wake, wakae mkao wa kupokea kibao hicho huku vingine vikiwa kwenye maandalizi.
Si mwingine bali ni yule nyota wa muziki wa Kizazi kipya hapa nchini, 'Abdukiba’ , kwa sasa anajipanga kufyatua goma  lake jipya linalokwenda kwa jina la ‘Dunia Mapito’, ambayo amemshirikisha kaka yake Ali Kiba.
“Kiukweli najisikia furaha sana kuona kazi zangu zinapendwa na mashabiki na nimeamua kumshirikisha Alikiba kwa kuona kama ni msanii mkubwa na anaelewa anachokifanya katika ‘game’,” alisema Abdukiba.
Mbali na kibao hicho, Abdukiba alishawahi tamba na vibao vyake kama; ‘Hatuna habari nao’, ‘Kizunguzungu’, ‘Huyo sio demu’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia hiyo.
Abdukiba, Ali kiba kupamba 'Dunia Mapito' Reviewed by Unknown on Wednesday, October 10, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.