Top Ad unit 728 × 90

BOB JUNIOR , "NIKO TAYARI KUSIMAMA NA DIAMOND"

Nyota wa ngoma ya mawazo ambaye pia  ni bosi wa lebo ya Sharobaro Record, ya  jijini Dar, Bob Junior amesema sasa yuko tayari kusimama kwenye ngoma  moja na mkali kutoka Wasafi Entertainments, Diamond Platinumz.

Akizungumza mapema jana  Bob Junior amesema licha ya kuwa aliwasiri juzi jioni   kutoka  Oman alikokuwa kwa mapumziko na amepata bahati ya  kuisikiliza  ngoma  mpya ya Diamond na kuona kuwa  ni kawaida kwani haina kitu kipya ilichofanyiwa

"Unajua kwa sasa mimi nimewapisha vijana wangu kwanza  watoa ngoma zao na baada ya wiki mbili nitatoa ya kwangu, ninachoweza  kusema ni kuwa sasa niko tayari kusimama kwenye wimbo mmoja na dogo huyo kwani  naamini mimi ni mkali zaidi yake na watanzania  wanajua hilo" alisema  Bob.

Akiendelea zaidi Bob aliyeitikisa Bongo kwa  ngoma kali ya Oyoyo alifunguka kuwa, sasa ana mipango ya kufanya  vitu tofauti vitavyosukuma mbele muziki wa  kizazi kipya na zaidi akilenga  katika  kujiongezea mapato tofauti na kutegemea  MKWANJA WA shoo au promo za matangazo.

BOB JUNIOR , "NIKO TAYARI KUSIMAMA NA DIAMOND" Reviewed by Unknown on Wednesday, October 31, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.