Top Ad unit 728 × 90

"HUWEZI KUNIPATA BILA KUWA NI MILIONI MOJA:......JACK WOLPER

WAKATI filamu nyingi za bongo bajeti yake si ile ya kushtua mtu kama kazi za wasanii wa mbele, na kwa kulitazama hilo msanii Jackline Wolper ameamua kuweka wazi fungu lake ili kwa wale wanaotaka kumshirikisha kwenye filamu zao basi wajue kuwa anaweza kucheza kuanzia milioni 1 na kuendelea chini ya hapo hapotezi muda.

Wasanii wa Tanzania wanatatizo kubwa la kutotumia pesa ya kutosha katika utengenezaji wa filamu zao, na wengi bajeti zao ni chini ya mil 8, hivyo kwa kiasi anachokitaka Wolper sijui kama ni kweli anaweza kulipwa ingawa wengi tumewazoea wakisema hivyo lakini mwisho wa siku unasikia kacheza filamu kwa laki 2.


Msanii huyo aliweka wazi ishu hiyo wakati akizungumza kwenye mahojiano na televisheni moja jijini al
iulizwa kiasi anachotaka kulipwa kucheza filamu, ndipo alipotaja fungu hilo.

“Kwa kweli suala la kulipwa mara nyingi huwa inatengemea na filamu yenyewe lakini kwa upande wangu naweza kusema kwamba kuanzia milioni 1 hapo nafanya kazi,”
alisema.

"HUWEZI KUNIPATA BILA KUWA NI MILIONI MOJA:......JACK WOLPER Reviewed by Unknown on Thursday, October 18, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.