Top Ad unit 728 × 90

JACO BEATS: Sijaacha Muziki na Siwezi kuacha Muziki!

Producer na Msanii anayekuja kwa kasi nchini Tanzania Jaco Beats a.k.a 'The Toucher' ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake yake ya 'I Say' aliyoiproduce yeye mwenyewe amekanusha madai kwamba ameacha muziki kutokana na mashabiki wake kumpigia simu nyingi na kumlaumu kwamba kwa sasa amepotea katika game kwani watu wamezimis ladha zake pamoja na production alizokuwa akizifanya hapo mwanzo kupitia studio za Wanyausi Records - Dodoma.

"Sijaacha Muziki na siwezi kuacha Muziki, japo ni kweli nilikaa kimya kwa kipindi kifupi hiyo ikiwa ni kutokana na mambo mengi kuingiliana na hasa kikubwa kuhama kwa Studio za Wanyausi ambazo kwa sasa zipo jijini Mbeya na ni nje ya uwezo wangu mimi kuendelea kufanya kazi kule kutokana na kwamba bado masomo yananiweka bize sana kwani nipo chuo Dodoma'. na kipindi chote ambacho nimekuw akimya nilikuwa Dar ambako nilikuwa nikifanya kazi na studio kama Dreams Rec ambayo ipo Ubungo na Wize Records ambayo ipo pande za Mbagala, na muda si mrefu nitaachia track yangu inayokwenda kwa jina la "Wife Material" pamoja na kazi nyingine nilizoproduce za wasanii ambao wako chini ya Campuni yangu mwenyewe ya "Peremende Music Tone" na nawaahidi mashabiki wakae tayari kuzipokea kazi hizo waone utofauti kwani kazi ni nzuri na zenye ubora wa hali ya juu'  

Alisema Jaco Beats.
JACO BEATS: Sijaacha Muziki na Siwezi kuacha Muziki! Reviewed by Unknown on Tuesday, October 16, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.