Top Ad unit 728 × 90

‘WITNES’ BAADA YA KUTAMBA KWENYE HIP HOP SASA AINGIA KWENYE MAIGIZO…!!

BAADA ya kufanya vizuri kwenye game la muziki wa hip hop miaka kadhaa nyuma na kupotea msanii ‘Witness’, ameibuka nchi kavu na amedai kuwa sasa anafanya maigizo na tamthilia na kwa upande wa muziki anapumzika kwanza ingawa hajafikilia kuacha kabisa kama watu wanavyodai.

Msanii huyo aliyewahi kutamba na ngoma kibao ikiwemo ‘Zero’, vile vile amesema kuwa ataendelea kufanya muziki lakini kwa sasa anapumzika na atakaporudi itakuwa ni fujo kwani kuna ngoma kadhaa ambazo ameshazifanyia kazi.

Hata hivyo mtandao huo ulitaka kujua anafanya maigizo chini ya kampuni gani ndipo alipodai kuwa yupo chini ya Mr Chuzi, ingawa bado hajaanza kuuza sura kwenye filamu yoyote.

“Sijafulia lakini nipo tu mjini kwani kwa sasa nafanya maigizo nipo chini ya Mr Chuzi na nipo keenye tasnia hii kwa sababu iiwango changu kinaniruhusu, pia kwenye upande wa muziki nitarudi wakati wowote,” alisema.

‘WITNES’ BAADA YA KUTAMBA KWENYE HIP HOP SASA AINGIA KWENYE MAIGIZO…!! Reviewed by Unknown on Friday, October 05, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.