Top Ad unit 728 × 90

Picha mbalimbali katika fainali za EBSS

Msanii Barnaba akiimba na mmoja wa washiriki wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),




Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Linah na Amin wakiimbwa kwa pamoja wimbo mpya uitwa Mtima Wangu


Ben Pol akimtuza Mshiriki na Mshindi baada ya kumkuna na kibao chake mwenyewe





Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Productions Limited, na jaji mkuu wa Shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS), akiwa amemkumbatia mshindi wa shindano hilo Walter Chilambo usiku huu ndani ya ukumbi wa Diamond,Chilamba ameibuka na kitita cha shilingi Milioni 50

Mshindi wa shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo (Dar) akikabidhiwa sanduku lake lenye kitita cha shilingi milioni 50 usiku huu ndani ya ukumbi wa Diamond jubilee,katika shindano hilo lililovuta hisia za wengi,mshindi wa pili ameibuka mwanadada Salma Abushiri  (Zanzibar) na watu ni Wababa Mtuka (Dar)

Mshindi wa shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo (Dar) akiwashukuru wapenzi na msahabiki wake waliompigia kura na hatimaye kuibuka mshindi wa shindano hilo,lililofanyika ndani ya ukumbi wa Diamond jubilee,usiku huu.

Baadhi ya mashabiki wa mshindi wa shindano hilo la EBSS,Walter Chilambo wakishangilia kwa shangwe na vifijo mara baada kutamkwa yeye ndiye kinara katika kilele cha shindano hilo lililovuta hisia za watu wengi





Mwasiti nae alikuwepo 'Mtoto anazidi kupendeza kila siku'


Mshiriki wa Epiq Bongo Star Search 2012 kutoka Dar-Es-Salaam Walter Chilambo usiku wa kuamkia leo amekuwa mshindi wa jumla wa shindano hilo na kujinyakulia kitita cha shilingi za kitanzania Milioni 50 kama zawadi ya mshindi wa kwanza.

Walter aliibuka kidedea mbele ya Salma Yusuf kutoka Zanzibar ambaye walifaikiwa kuingia naye pamoja fainali ya washiriki wawili tu kati ya watano ambao walianza fainali hiyo hapo awali. Walter ambaye dalili za ushindi wake zilianza kuonekana tangu awali mwa fainali hiyo ameweka historia ya kuwa mtanzania wa kwanza kujinyakulia kitita kikubwa katika mashindano ya kusaka vipaji vya muziki.

Aidha katika shindano hilo la kuamkia leo mshiriki Walter pamoja na wenzake walipitia hatua tatu ambapo ya kwanza ilikuwa kuimba na msanii mmoja mmoja waliowachagua ambapo yeye aliimba na msanii Ditto kabla ya kuimba mwenyewe katika raundi mbili zilizofiuata huku wakipigiwa kura na mashabiki katika raundi zote. 

Walter alitumia nyimbo moja ya Steve R n B “One Love”, na Nikikupata ya Ben Pol katika raundi zote mbili zilizofuata.
Picha na Habari kwa niaba ya 'mpekuzi.blogspot'
Picha mbalimbali katika fainali za EBSS Reviewed by Unknown on Saturday, November 10, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.