Top Ad unit 728 × 90

Rihanna atangaza nchi saba atakazopiga tour yake ‘777’

The Diamond hit maker ametangaza rasmi ratiba ya tour yake iliyokuwa inasubiriwa sana na fans wa nchi kibao ikiwa na title ‘777’ ikiwa na maana ya nchi saba, siku saba na show saba atakazopiga. 

Rihanna anatarajia kuzunguka na jet maalum kwa siku zote saba na anatarajia kuambatana na group la watu 150 ambao ni waandishi wa habari na fan club members ambao watazunguka nae katika nchi zote saba. 

RiRi mwenyewe alifunguka, “I am so excited about the 777.” Mrembo huyo mwenye miaka 24 aliendelea kuonesha furaha yake kuhusu 777 tour, “tunaibadili hii Jumbo Jet kuwa bus letu la tour. Tutaishi ndani ya hiki kitu kwa wiki: kulala, kuparty, vyote kwa pamoja. Mimi, fans wangu, waandishi wa habari...it is going to be a wild ride.” Rihanna anasema anataka kuwa rock and roll adventure katika tour hiyo. 

The R&B Diva alionekana kuipania sana tour hiyo kiasi cha kuwafanya fans waombe majina la nchi zao yawe kwenye hiyo list ya nchi saba, “nadhani ni kitu poa zaidi ya kitu chochote nichowahi kufanya. I’m that excited about it,” alisema Rihanna. 

Wakati Rihanna anajiandaa na tour hiyo, album yake ya saba ‘Unapologetic’ inasubiri kuachiwa officially November 19. Ikiwa na ngoma yake ya kwanza aliyoiachia ‘Diamonds’ na ‘Stay’ aliyoiachia hivi karibuni.

Hii ndiyo ratiba ya ‘777’ tour ya Rihanna kwenye nchi saba kwa siku saba na show saba:

•             November 14 in Mexico City
•             November 15 in Toronto
•             November 16 in Stockholm
•             November 17 in Paris
•             November 18 in Berlin
•             November 19, Worldwide Album Release Date, in London
•             November 20 in New York City


Rihanna atangaza nchi saba atakazopiga tour yake ‘777’ Reviewed by Unknown on Wednesday, November 14, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.