Top Ad unit 728 × 90

RZA asema kufanya kazi na Wu Tang Clan kumemtengenezea njia ya kuwa director bora.

Akiwa amehusika kwa asilimia mia kuongoza documentary film ambayo inategemewa kupata mafanikio makubwa katika mauzo na kila kitu “The Man with the Iron Firsts” aliyekuwa kiongozi wa kundi la Wu Tang Clan, RZA anategemewa kuwa mmoja kati ya wakali watakaokuwa wanatoa michango yao nyuma ya kamera kama waongozaji kwenye film industry Hollywood. 

Akipiga interview na Ruby Hornest kwenye kipindi cha “Rubyhornest’s coffee with RZA”, mkali huyo amesema nyakati zake kama kiongozi wa Wu Tang Clan ndizo zilizomjenga na kumfanya leo akae kwenye kiti kama muongozi (Director). 

Amesema kufanya kwake kazi kama kiongozi ndani ya kundi la watu zaidi ya nane kulimfanya ajifunze namna ya kuzungumza, kutreat na kuweka mambo sawa pale yanapokuwa hayako sawa ili aende sawa na washkaji zake na kisiharibike kitu, na sasa kama muongozaji wa filamu anahakikisha anakuwa fresh kwa waigizaji na mafundi mitambo pia ili mambo yote yaende sawasawa. 

“Wu Tang kiukweli ilikuwa ni funzo zuri sana ambalo sitakuja kulipata tena, sikuwa muelewa kiasi cha kukubali kila pitio langu nyakati mbaya na nyakati nzuri nikiwa na Wu Tang ndo imepelekea niwe nilivyo leo, niwe natazama usanii na vipaji lakini kitu kimoja kikubwa ambacho kimenisaidia ni kwamba mimi ni msanii naelewa njia zote, naelewa kwanini sasa hivi tunatoka mapema na kuiwahi mvua tunakaa hapa na kuzungumzia filamu hii badala ya kukaa kwenye basi...tukivuta joto naelewa inavyokuwa nathamini kitu ambacho msanii anakifanya. Kuna baadhi ya nyakati tulikuwa na matatizo…baadhi ya producers walikuwa wanataka kulipua tu…mi nikasema hapana…hauwezi kulipua tu…ni lazima kuwe na utayari kwanza” amemaliza RZA.
RZA asema kufanya kazi na Wu Tang Clan kumemtengenezea njia ya kuwa director bora. Reviewed by Unknown on Thursday, November 15, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.