Top Ad unit 728 × 90

UKWELI WA DJ CHOKA KUHUSU TATOO YAKE YENYE JINA LA PROF JAY

Baadaya kujichora tatoo yenye jina la Prof Jay na kupost picha yake akionesha tatoo hiyo katika mitandao ya kijamii Twitter na Facebook na hatimae mashabiki wake kuwa na maswali mengi juu ya tatoo hiyo Dj CHOKA ameamua kuweka wazi ni kwa nini ameamua kuchora tatoo hiyo..

"NDUGU ZANGU NIMESOMA COMMENTS ZENU NA NIKAWAELEWA SANA SIWEZI PINGA MAWAZO YA WATU OK. Sasa ni hivi nia na dhumuni la kuchora tattoo yenye jina la PROF JAY ni kwamba nusu ya maisha yangu yote mpaka kufika hapa nakuwa na familia yangu yeye ndio nguzo yangu imara na nuru ya ushauri wangu kila siku iendayo kwa mungu. Na kama mlikuwa hamjui me sio shabiki wa PROF JAY mimi ni ndugu na nimdogo ambaye wazazi wangu waliponiruhusu kulelewa na Prof Jay ndio nikaanza kufundishwa huu mziki wa bongo mpaka sasa nimekuwa na kusimama mwenyewe. So tattoo hii ni heshima ambayo haitofutila milele mpaka nakufa na why umsifie mtu akisha kufa? Nampa heshima yake akiwa hai ili ajue kwamba huu wino unamaana nyingi sana. Natukuza vya nyumbani vya nje sivijui kiundani...ASANTENI"

Hayo ndo yaliyosemwa na DJ CHOKA katika ukurasa wake wa FACEBOOK..
UKWELI WA DJ CHOKA KUHUSU TATOO YAKE YENYE JINA LA PROF JAY Reviewed by Unknown on Saturday, November 17, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.