Top Ad unit 728 × 90

Jay Mo ajuta kuchelewa kufanya kazi na Dimpoz, Kiba na Diamond

Msanii Mohamaed Mchopanga almaarufu kma Jay Mo amesema kwa sasa anatamani sana kufanya nyimbo na wasanii Ommy Dimpoz, Ally Kiba na Diamond baada ya kubaini wanakubalika sana Ulaya kwa kazi ambazo tayari wameshazitoa. Akipiga stori na baadhi ya wadau katika utengenezaji wa video ya nyimbo na kundi la No Name; juzi katika viwanja vya Tanesco eneo la Msasani Dar es Salam, Jay Mo alisema baada ya kufika Uholanzi na pia kutembelea nchi nyingine kadhaa aligundua namna wasanii hao watatu walivyo na mashabiki wengi, baada ya kuulizwa mara kwa mara kuhusiana na wasanii hao. Ningekuwa nimefanya kazi na mmoja kati ya hawa wasanii au wote nafikiri ningekuwa na mashabiki wengi zaidi, maana hawa wasanii wanakubalika sana kule. Tunamnukuu “Nafikiri nipo kwenye hatua nzuri ya kufanya kazi na wasanii hao watatu na wa kwanza ambaye naweza kukiri nimeona muitikio wake ni mkubwa ni Ommy Dimpoz ambaye tangu nimwambie kuhusiana na ishu hii amekuwa akiniuliza mara kwa mara lini tunaingia studio” alisema Jay Mo.
Jay Mo ajuta kuchelewa kufanya kazi na Dimpoz, Kiba na Diamond Reviewed by Unknown on Tuesday, December 04, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.