Top Ad unit 728 × 90

NASH MC KUANZA KUUZA SINGLE KUANZIA 2013

Msanii Nash MC au Maalim Nash ameweka wazi malengo yake kwa mwaka unaofuata kwamba anatarajia kuanza kuuza muziki wake kwa mtindo wa Track Moja moja ama single. Hii imetokana na kwamba amechunguza vizuri na kuona watu wanaupenda muziki wa hip hop kwa hiyo badala ya mashabiki kwenda kwenye vibanda vya kuchoma CD sasa kutakuwa na utaratibu ambao atautumia yeye kuziuza single zake kupitia Internet.

Ameyasema hayo kwa kuongeza kuwa atakuwa akiweka kipande kifupi cha nyimbo katika mtandao ili wapenzi wake wapate kusikiliza na mtu akiupenda wimbo husika basi anawasiliana naye na kutumiwa wimbo huo kwa e-mail.

Pia ameweza kukitaja kiwango au gharama za wimbo mmoja kuwa utakuwa unauzwa kwa shilingi za kitanzania (Mia Sita) 600/= tu na kudai bei hii inalipa kutokana na kwamba Album inauzwa elfu 3 hadi 5 kwa hiyo ukilinganisha bei ya Tshs 600 kwa kila wimbo bado msanii ataweza kujipatia faida katika kazi zake.

Nash MC amewaomba sana mashabiki wake waweze kum-support kwa ujio wake huo mpya wa kuuza Single ama wimbo mmoja mmoja katika internet.
NASH MC KUANZA KUUZA SINGLE KUANZIA 2013 Reviewed by Unknown on Wednesday, December 26, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.