Top Ad unit 728 × 90

MSIBA MWINGINE WA MSANII WA MUZIKI NCHINI OMARY OMARY

MSANII nyota wa miondoko ya Mnanda a.k.a Mchiriku, Omari Omar amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu. Habari zilizoifikia , asubuhii zinasema kuwa, Omar Omar aliyetamba na nyimbo mbalimbali ukiwemo ule maarufu wa 'Kupata ni Majaliwa' alifariki nyumbani kwao Temeke, saa chache baada ya kurejeshwa toka hospitali ya temeke alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.

Taarifa hizo zinasema kuwa mara baada ya kurejea nyumbani, msanii huyo alizidiwa na hatimaye kufariki na kwamba msiba wake upo nyumbani kwao Temeke Mikoroshini kwa ajili ya mipango ya mazishi. Msiba wa msanii huo umekuja siku chache baada ya tasnia ya sanaa na burudani kumpoteza Juma Kilowoko 'Sajuki' msanii nyota wa filamu aliyefariki pia kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya muda mrefu.

Akielezea kifo cha msanii huyo Mkubwa Fella ambaye ni jirani yake amesema marehemu Omari Omari alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua.

Dj Mchomo blog inawamuombea kila la heri Omar Omar na wengine waliotangulia mbele ya haki mapumziko mema katika safari yao ya Ahera.

MSIBA MWINGINE WA MSANII WA MUZIKI NCHINI OMARY OMARY Reviewed by Unknown on Tuesday, January 08, 2013 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.