Watu kumi na tatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma kwa tuhuma za mauaji yanayohusisha imani za kishirikina.
TAARIFA KWA VYOMBOO VYA HABARI
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI
TANZANIA
YAH: TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA
DODOMA KWA
VYOMBO VYA HABARI TAREHE 10/01/2013.
Watu kumi na tatu
wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani
Dodoma kwa tuhuma za mauaji yanayohusisha imani za kishirikina.
Watu hao
wanashikiliwa kutokana na tukio la mauaji lililotokea siku ya Jumatano tarehe 09/01/2013
majira ya saa 04:00 mchana katika kitongoji cha Mtakuja kata ya Chitemo katika Wilaya ya Mpwapwa.
Katika tukio hilo walisababisha kifo cha mtu mmoja aliyefahamika
kwa jina la NELSON S/O NYAGULU mwenye umri wa miaka 32, mkulima wa Chitemo kwa kupigwa na risasi ya Bunduki aina ya
Gobore tumboni na mtu aliyefahamika kwa jina la RASHID S/O KALANI.
Uchunguzi
wa awali unaonyesha kwamba tarehe 08/01/2013 huko katika kijiji cha Chitemo
kulikuwa na mnada, ambapo mvua ilinyesha sehemu moja ya kitongoji cha Mtakuja,
sehemu ambayo alikuwa anaishi mzee mmoja
aliyejulikana kwa jina la LEONARD S/O NYAGALU, Miaka 70, Mgogo.
Kwa vile
mvua hiyo haikunyesha sehemu kubwa katika kitongoji hicho inasemekana
Mwenyekiti wa Kijiji JAVAN S/O MZAZI, Miaka 40, Mgogo, aliibua hoja kuwa kwa nini
mvua inyeshe eneo moja tu analokaa Mzee huyo na kuacha kunyesha sehemu nyingine
katika eneo hilo na kuwahamasisha wenzake kwenda kwa Mzee Nyagalu akawaeleze
vizuri.
Majira ya
23.00 hrs usiku wakakusanyana na kuelekea kwa Mzee Nyagalu, Walipofika Mzee huyo alisikia watu
wakizungumza nyumbani kwake hivyo akavunja ukuta na akatoroka.
Inadaiwa
kuwa kundi hilo lililokuwa limeongozana na Mwenyekiti wa Kijiji hicho waliingia
ndani ya nyumba na kumkuta mke wa Mzee Leonard Nyagalu na kuanza kumpiga ili
aonyeshe aliko mume wake, waliposhindwa kumpata wakabomoa nyumba na kuichoma
moto.
Wakati wanafanya
tukio hilo, walijitokeza watoto wa Mzee Leonard S/O Nyagalo, mmoja wao akiwa ni
NELSON S/O NYAGALU, Miaka 32, Mgogo na ndipo nao wakaanza kupigwa.
Kwa
mujibu wa watu walikuwa katika tukio hilo walisema ilisikika sauti ya mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la RASHID S/O KARANI akisema sasa mmetangaza vita na
akafyatua gobore na risasi zikampata NELSON S/O NYAGALU tumboni zilizopelekea
kupoteza maisha wakati anapata matibabu.
Baada ya
kufyatua risasi toka katika gobole Bw. RASHID S/O KARANI aliwaaga wenzake kuwa
anakwenda kujisalimisha Polisi lakini hadi sasa hajaonekana na jitihada za
kumtafuta pamoja na silaha aliyotumia zinaendelea.
Majina ya
wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na kushiriki katika tukio hilo ni kama ifuatavyo:-
1. Dickson
S/O Chimosa, Miaka 52, Mgogo, Mkulima na Mkazi wa Chitemo.
2. Javan S/O
Mzazi, Miaka 44, Mgogo, Mwenyekiti wa Chitemo.
3. Robert
S/O Lusije, Miaka 51, Mgogo, Mkulima na mkazi wa Chitemo.
4. Donald
S/O Mponi, Miaka 33, Mgogo, Mkulima na mkazi wa Chitemo.
5. Daniel
S/O Mwamba, Miaka 24, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
6. Maneno
S/O Ngaile, Miaka 36, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
7. Thomaso
S/O Nyagalo, Miaka 28, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
8. Gilbert
S/O Lugaje, Miaka 39, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
9. Aden S/O
Simon, Miaka 33, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
10.
Malolo S/O Sanja, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa
Chitemo.
11.
Sospeter S/O Sanja, Miaka 35, Mgogo,
Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
12.
Jocktan S/O Chilomo, Miaka 40, Mgogo,
Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
13.
Keneth S/O Ngaile, Miaka 38, Mnyamwezi,
Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
Aidha
siku ya Jumamosi tarehe 05/01/2013 majira ya 08:00 asubuhi kulikuwa na
tukio la mauji lililotokea katika
Kitongoji cha Magungu, Kijiji cha Mpendo, Kata ya Mpendo Tarafa ya Kwa Mtoro
Wilaya ya Chemba Mkoa wa Dodoma.
Ambapo mtoto mmoja
aliyetambulika kwa jina la TONY S/O SOKOINE mwenye umri wa miaka miwili na nusu
(2.5), mkazi wa Kijiji cha Mpendo alifariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa
kuchomwa na kisu shingoni kilichorushwa na mtoto mwenzake aliyefahamika kwa
jina la SOMEI S/O REMENDA mwenye umri wa miaka mine (4) mkazi wa Kijiji cha Mpendo.
Uchunguzi wa awali
unaonyesha kuwa chanzo cha Kifo hicho ni kwamba marehemu na mtuhumiwa walikuwa
wanacheza nje nyumbani kwao kwa akina SOKOINE S/O RENENDA ambapo mtuhumiwa
alirusha kisu kwa lengo la kumuua ndege aliyekuwa juu ya mti uliokuwa karibu na nyumba yao, ndipo kisu
huchi kiligonga kwenye mti huo na wakati kinadondoka kilimjeruhi marehemu kwa
kumchoma shingoni na kusababisha kifo
chake.
DAVID A. MISIME - ACP
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA DODOMA
Watu kumi na tatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma kwa tuhuma za mauaji yanayohusisha imani za kishirikina.
Reviewed by Unknown
on
Thursday, January 10, 2013
Rating:
No comments: