KALA PINA NA NASH MC WAELEZA NINI CHANZO CHA KUPIGWA KWA CHID BENZ
Baada ya muasisi wa harakati za hip hop Tanzania Kalapina kumchapa
Rapper Chidi Benz katika jukwaa la maisha club hapo jana,
Kalapina ameelezea sababu za kutoa dozi hiyo kwa msanii mwenzake,
hichi ndicho alichosema: " ukweli ni mambo fedheha, mdogo wetu chidi benzi cocaine au
heroin / unga anaovuta unampeleka pabaya, tena mimi kama kaka yake
namshauri aachane na matumizi ya madawa kulevya, kwa sababu mwisho wake
utakua m'baya, mimi nilikua back stage na ikafika zamu yangu kupanda
jukwaani nikawa naskia sauti mtu anatamba jukwaani kwa dakika saba ama
nane, alikua ananichelewesha kupanda, na ananiharibia show yangu, huyu
mtu si adui, nikatoa amri mara tatu kama F.F.U aka kaidi ndipo nikamfata
na kumpa dozi, akaanguka chini na mimi nikaendelea na show yangu,
hakuna hata mtu mmoja atakaye kubali kuharibiwa kazi, hata rais Kikwete
ukimharibia utaishia jela."
Pia Msanii NASH MC a.k.a Kaka Suma nae pia aliweza kutoa maoni yake kuhusiana na sakata hilo kwa kuwaeleza watu kile kilichotokea ili watu waweze kufahamu yupi hasa alikuwa kinyume na mwenzie hadi kusababisha ugomvi huo; Nash aliandika maneno haya katika ukurasa wake wa facebook."
Hapa chid Benz ndo alishaanza kuharibu mambo jukwaani kitu kilichopelekea mtata Kalapina kumfuata na kumpa kichapo |
KALA PINA NA NASH MC WAELEZA NINI CHANZO CHA KUPIGWA KWA CHID BENZ
Reviewed by Unknown
on
Tuesday, May 07, 2013
Rating:
No comments: