Top Ad unit 728 × 90

KALA JEREMIAH AKABIDHI TUZO YAKE YA MSANII BORA WA HIP HOP KWA ALBERT MANGWEA

Katika ukurasa wake wa FB leo msanii Kala Jeremiah ametoa taarifa hii kwa vyombo vya habari nchini kuhusiana na tuzo zake tatu alizokabidhiwa mwaka huu.

"TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA KWA UJUMLA.

MIMI KAMA MSANII BORA WA HIP HOP KWA MWAKA HUU NAPENDA KUCHUKUA MUDA HUU KUWATANGAZIA WATU WOOTE KUWA. KATIKA TUZO TATU NILIZOCHUKUA MOJA NAIKABIDHI KWA ALBERT MANGWEA.YANI NI TUZO YA MANGWEA NA NITAIPELEKA KWA MAMA MZAZI WA MANGWEA MOROGORO.

NIMEAMUA HAYO KWA KUWA HAYATI ALBERT MANGWEA ALIKUWA ANAFANYA MZIKI AMBAO UKO UPANDE AMBAO MIMI NIMESHINDA TUZO TATU YANI HIP HOP.

TUZO NILIYOAMUA KUMPA MANGWEA NI TUZO YA MSANII BORA WA HIP HOP. KWA KUWA ALIKUWA ANASTAHILI PIA KUITWA HIVYO.

TUZO HII NAAMINI ITAKUWA UKUMBUSHO MHIMU SANA KWA FAMILIA YAKE.LAKINI PIA ITAKUWA INAONYESHA MSHIKAMANO WETU KAMA WASANII WA HIP HOP.

POPOTE ULIPO KAMA WEWE NI SHABIKI WA HIP HOP TAFUTA NJIA YOYOTE YA KUENDELEA KUMUENZI NDUGU YETU

MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI HIP HOP'.

Alimaliza kwa kusema hayo KALA JEREMIAH
KALA JEREMIAH AKABIDHI TUZO YAKE YA MSANII BORA WA HIP HOP KWA ALBERT MANGWEA Reviewed by Unknown on Tuesday, June 11, 2013 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.