KWANINI NASH ALIJIITA ''MC''?,NANI ''MC'' WA KWANZA,NA NI NANI ALIANZA TUMIA NENO ''MC'' KATIKA HIPHOP?
Naam! sikufikiri na sikudhani kama nilikuwa mwenye makosa makubwa pale
nilipokumbuka kuwa mimi ni miongoni mwa watu wenye kuutakia mema
utamaduni huu wa HIPHOP kila kukicha kwa kadri nilivyojaaliwa,lakini
kutokujuta kwangu moja kwa moja nikiwa nimejiegesha katika kikochi na
sauti ya wastani ya ghani mahiri toka kwa wachenguaji bora walionifanya
nigeuke teja wa kusikiliza iliingia katika ngoma za masikio yangu.
Vibao vyao na mitambao yao vyote viliendelea chakatwa na ubongo wangu
vyema na moja kwa moja vikanisanisafirisha mpaka kwenye kitabu maridhawa
kabisa kuhusu utamaduni huu wa HIPHOP nikapenyeza kidole na kwenda
kubisha hodi kwenye ukurasa ulioandikwa yaliyomo nao moja kwa moja
ukanielekeza ukurasa wa 47 ambapo nilijazwa unene wa maarifa
nilipogundua kuwa kilichozungumzwa hapo ni NGUZO ZA HIPHOP,ambapo hapo
wengi walijimwaya na kutaja idadi ya NGUZO ZA HIPHOP mfano,
TOVUTI YA URBAN DICTIONARY
Ilitoa idadi ya nguzo kama tisa (9)kwa idadi yake kama
Mcing,d-jaying,battlelling,graffiti,B-boying,Beat boxing,The
style(fashion),The slang,rope skipping,pia hawa hawakubaki nyuma.
WIKIPEDIA.
Mtandao huu ulitoa hizi Mcing,d-jaying,break dance,na graffiti,beat
boxing,lakini katika hizi Mwanaharakati AFRIKA BAMBATAA alizitaja zote
kasoro beat boxing,sasa nkajiuliza
JE KUNA NGUZO NGAPI ZA UTAMADUNI HUU?
YOUTH ETHICS INITIATIVE INC kwa ushirikiano na CHUO KIKUU CHA MIAMI.
Walisema kiasilia kulikuwa na nguzo nne (4) yaani Uchenguaji,umanju,uvunjaji,machata lakini nguzo ya tano ''Maarifa''ikaongezeka
Swadkta kabisa kuangalia muda nikiwa safari nilijikuta nkigonga mlango
(ukurasa) nambari 48 palipodadavuvuliwa nguzo ya maarifa kwa heshima
kabisa nikaisoma na kuhitimisha katika kutafuta mengi pitia vyanzo
mbalimbali nikazidi ingia ndani ya milango hiyo nikajikuta nikigonga
mlango nambari 54,56 na 58.na kuwaleteeni haya.
NANI ALIKUWA ''MC'' WA KWANZA?
Ni swali zuri lakini wengi tunaopenda HipHop hatufahamu kama ni
kweli,narudi palepele kwamba tafuta ufahamu/maarifa (Knowledge)kama mimi
ninavyojaribu pindi panapopatikana upenyo ama muda,safi jibu la swali
ni kwamba ingawa inaaminika kuwa COKE LA ROCK ndiye aliyekuwa mchenguaji
wa kwanza wa HIPHOP lakini si wa kwanza kuanzisha neno ''MC''sasa.
JE NANI ALIANZA TUMIA NENO HIPHOP?
Ndiyo,swali mezani kama tulivyoona hapo juu kuwa Bw.Coke La Rock ndiye
mgahanaji wa kwanza lakini hakulitumia neno ''MC''katika kujiita na
kuliingiza katika utamaduni wa HipHop kwa kina lakini MELLE MEL
huyu anageuka kinara wakuliingiza neno hili katika Hiphop,ndugu huyu
aliyezaliwa huko South Bronx jijini New York,Marekani mwaka 1961,alileta
athari kubwa katika utamaduni wa HIPHOP kwa kuleta mitindo mbalimbali
ya ghani,Mchenguaji wa HipHop wa kwanza kupata tunzo ya Grammy,pia kibao
chake kiitwacho ''The Message'' ndicho cha kwanza katika utamaduni wa
HipHop kuingia katika kumbukumbu za taifa za vibao vya kihistoria (United States National Archive of Historic Recordings),toka katika hili ndipo laja hili.
JE KWANINI NASH ALIJIITA ''MC''?
Katika tafsiri zoefu neno ''Mc'' ni mchenguaji au mshereheshaji au kwa kimombo yaweza andikwa kama ''Master of ceremony''kwa
maana ya kuwa muongoza hafla ama sherehe au tumbuizo,akhsante sidhani
kama nimetukana katika hili lakini naamini kuwa majina yetu mengi
tumerithi kwa wale tulowakuta kwa lengo la kuwaenzi au mapenzi
yetu,hivyo kama mistari kadhaa hapo juu ilivyoeleza kuwa MELLE MEL
ameacha athari ya mitambao mingi kwa wale waliomfatilia/mashabiki wake
hivyo hata jina au neno ''MC'' limekuwa chachu kwa Wanahiphop wengi
kujiita mfano,leo tuna NASH MC,P THE MC na wengine wengi pia,lakini
athari hizi haziishii tu katika majina bali athari kwa Waghanaji wengi
wanaomkubali na kumuelewa Melle Mel,mfano hapa.
Nash MC anasema ''Melle Mel ni mtu wa kwanza kudondosha
mistari mitamu,ule utamu wa mistari umeanzia kwa huyu mtu''.
Hivyo sasa nakumbuka usemi usemao mwisho wa kizuri cha leo ni mwanzo wa
kizuri cha kesho,ndugu zangu katika utamaduni huu naomba niwaache
mkiperuzi haa machache niliyowaandaleni,AMANI KWENU.
(shukrani,(REJEA,Hanzi,M.S,Chuo Kikuu Cha HipHop(2012),Ubunifu Wetu
Printing Press,Dar Es Salaam)uk,54,56 na 58.
WAKO,Amri Mlela/Niite Maalim (0654 30 40 30).
Chanzo: nashemcee.blogspot.com
KWANINI NASH ALIJIITA ''MC''?,NANI ''MC'' WA KWANZA,NA NI NANI ALIANZA TUMIA NENO ''MC'' KATIKA HIPHOP?
Reviewed by Unknown
on
Friday, September 27, 2013
Rating:
No comments: