Top Ad unit 728 × 90

Mrembo toka Dodoma Happiness Watimanywa anyakua Taji la Redd's Miss Tanzania 2013

Hatimaye Mrembo toka Dodoma Happiness Watimanywa amejinyakulia taji la Redd's Miss Tanzania ambali limefanyika usiku wa kuamkia lea Mlimani City Dar es Salaam na kuuwakilisha mkoa wa Dodoma vizuri tofauti na miaka mingine ambapo tumezoea kuona warembo wakitokea katika vitongoji vya jiji la Dar es Salaam.
Chini ni picha za Mashindano hayo toka Happiness Watimanywa akiwania taji hilo Dodoma hadi Dar es Salaam ambapo nako amedhihirisha kuwa alikuwa amepania na hata majaji waliomchagua toka Dodoma kuwa anafaa watajivunia hilo kutokana na kutoa mshindani mwenye sifa za kitaifa na hata kimataifa kwani ndiye atakayeiwakilisha nchi katika mashindano ya Dunia huku mimi binafsi nikimpa sifa za kufanya vizuri kataika mashindano ya Dunia.

Happiness Watimanywa huku ndiko alikoanzia ambapo hapa alikuwa na vazi la ubunifu kipindi hicho mkoani Dodoma
Hawa ni Majaji waliomchagua Happiness Watimanywa toka Dodoma ambako walimfungulia njia nzuri hadi kukubalika na taifa zima kuwa anafaa kuwa mrembo wa kitaifa na kimataifa...Big Up meza hii naikubali sana
Tazama Picha za chini ambazo ndio za fainali hizo kitaifa jijini Dar es Salaam



Hii ni kumi na tano bora ambapo ndipo mchujo ulipoanzia
Hapa ni warembo waliotangazwa kuingia tano bora
Happiness Watimanywa akiwapungia mkono mashabiki mara baada ya kutangazwa na kuvikwa taji hilo kushoto ni Mshindi wa Pili Latifa Mohamedi na Mshindi wa Tatu kulia Clara Bayo

Mrembo toka Dodoma Happiness Watimanywa anyakua Taji la Redd's Miss Tanzania 2013 Reviewed by Unknown on Sunday, September 22, 2013 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.