Top Ad unit 728 × 90

SHEBBY LOVE & NAY WA MITEGO KATIKA NGOMA YA PAMOJA TENA

Baada ya kipindi kirefu kutoka na ngoma ya pamoja wakiwa na Matonya, na kutokea kutokuelewana baina yake Shebby Love na Nay wa Mitego wanarudi tena na maandalizi ya ngoma nyingine inayokwenda kwa jila la "Nilimuona kwenye Runinga" ambayo itasimamiwa na Producer mahiri nchini Mr T Touch ndani ya studio zake za Seductive Record zilizopo jijini Dar es Salaam.
 
Kwa mujibu wa Shebby Love mwenyewe amedai kwamba kwa sasa wamemaliza tofauti zao na wameamua kutazama mbele kwa ajili ya kuendeleza game yenye maslahi zaidi na kudai kuwa ngoma hiyo ni hatari sana na mashabiki wakae mkao wa kuipokea kwani ana uhakika na kazi zake hasa anapokutana na Nay pamoja na Mr T Touch huwa hawabahatishi.
 
Ngoma inatarajia kutoka mapema mwaka huu ambapo kwa sasa Shebby Love anakimbiza na wimbo wake mpya Ndo wale wale' wakati Mbabe Nay yeye anaendelea kula ujana na kumfanya awe juu wakati wote.

SHEBBY LOVE & NAY WA MITEGO KATIKA NGOMA YA PAMOJA TENA Reviewed by Unknown on Saturday, January 11, 2014 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.