Top Ad unit 728 × 90

Baghdad & Byter ft Cilubus & Jo Gift - Ni Shida [Audio]


Ni muda wa siku zisizopungua 200 tangu niachie nyimbo yangu ya waambie nipo iliofanywa na muandaaji mdogo wa muziki kiumri kati ya waandaaji wachache Tz ambao kwa sasa wanafanya kazi katika studio ya A.T, nyimbo ya waambie nipo ilikuwa ni moja kati ya nyimbo ambazo zilizofanya kuwashangaza wapenzi wa mziki walio wengi kwa kuwashirikisha maasimu wawili ambao kwa sasa sio maasimu tena na moja kati ya kitu kilichofanya wapatane Chidi Benz na Ney wa Mitego ni nyimbo ya waambie nipo! Mafanikio Baghdad aliyoyapata kutoka kwenye nyimbo hiyo ilimfanya aweze kusogea na kufanya nyimbo nyingine ambazo aliamua  kurecord kwa muda kisha kuanza kuziachia.

Siku ya Jumamosi Baghdad alikuwa location na team ya Vipaji Tz Rec Label ambayo inawamiliki Waswazi wasanii ambao wanatamba na nyimbo yao ilioachiwa video mwez wa 11 mwaka 2013 iitwayo Your Noumber, Baghdad amesema vipaji tz ni recd laba ninayofanya nayo kazi kwa sasa hivyo nafanya kazi na waswazi jumla tuko 9 muandaaji mmoja ajulikanae kwa jina la Abba Prosess na wasanii 8 wasichana 3 na wavulana 4, Vipaji Tz.
Kwa sasa bado tunajikongoja lakini tuna mwanzo mzuri ingawa ni mgumu kwa sababu nyimbo ya Waswazi ya Your Noumber imefanikiwa kuchanua miamba katika vituo vikubwa vya TV vya ndani na ne ya nchi, aidha nachomchukuru Mungu Vipaji Tz ina makazi kigogo Dar es Salam ambayo ina makazi ya wasanii walioko chini ya Rec Label ya Vipaji Tz na studio ndani, namshukuru mungu kwa kuwa nyimbo tulizoziandaa ni nzuri na ni heat song zote na ninauhakika wasanii wanayoiunda ngome ya Vipaji Tz ni wasanii ambao kila msanii anaimba mziki tofauti na mwenzake. Kwa sasa tunaanza na project ya kwanza ambayo imepewa jina la Non Stop ambayo kila wiki tutakuwa tunaachia nyimbo moja audio and video, tar 7 tutaanza na nyimbo inayoitwa ni shida ambayo imeunganisha Baghdad, na wasanii watatu kutoka Vipaji Tz Cilubus, Byter, na the only women Chourus Kiler Iron Lady cal her Jo Gift.

Nyimbo itakwenda sokoni Jumamosi ya tar 8 kwenye Radio na tar 7 kwenye vituo vya TV vya ndani na nje ya nchi aidha Baghdad ametoa ombi moja kwa wadau 'wadau nyinyi ndio mmenifanya kufika nilipofika  na nyinyi ndie ambao mnaweza kuamua msanii kufika au kutofika kwa niaba ya Vipaji Tz ninawaomba mtusaport ili tufikie malengo yetu tunaikabidhi Vipaji Tz kwenye mikono yenu kwenye zuri tupongezane na kwenye mapungufu turekebishane, kwa kumalizia Baghdad ametaja majina ya wasanii waliokochini ya Rec Label ya Vipaji Tz Cilubus, Jo Gift, Byter, Herieth, Ninja, Dream, Lovness, Baghdad na Produser wao aitwae Abba Prosess. Mungu ibariki Vipaji Tz, Mungu bariki Bongo Flavour

Song ; Ni Shida 
Artist ; Baghdad & Byter Ft Cilubus & Jo Gift
Studio ; Vipaji Tz
Producer ; Abah Process

Baghdad & Byter ft Cilubus & Jo Gift - Ni Shida [Audio] Reviewed by Unknown on Tuesday, February 18, 2014 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.