Top Ad unit 728 × 90

Miss Tanzania Happiness Watimanywa akabidhi taji la Urembo wa Kanda ya Kati kwa Mshindi Mpya 2014. [Habari & Picha]

Mashindano ya kumtafuta mrembo wa Kanda ya kati yamefanyika usiku wa kuamkia leo tar. 21.06.2014 katika ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma ambapo mshindi wa mashindano hayo yaliyoshirikisha warembo kadhaa toka mikoa mitatu ya Dodoma, Singida na Tabora amepatikana.
 
Kinyang'anyiro hicho kilileta ushindani mkubwa hasa ukizingatia kwamba washiriki toka mikoa yote walijipanga vya kutosha na kikubwa wote walikuwa ni washindi walioiwakilisha mikoa yao.
 
Mrembo Dorice Molel toka Singida ndiye aliyenyakuwa taji hilo akifuatiwa na mshindi wa pili 'Zena' toka Tabora na wa tatu 'Adelaida' toka mkoani Dodoma.
Meza Kuu ya Majaji



Wazazi wake na Miss Tanzania Happiness Watimanywa nao walikuwepo kushuhudia kinyang'anyiro hicho




Naibu waziri wa Michezo, Vijana, Habari na Utamaduni Juma Nkamia akifungua mashindano hayo 


Washindi hawa watatu ndio watakaowakilisha Kanda ya Kati katika mashindano ya urembo ngazi ya Taifa yaani Miss Tanzania 2014/2015.
 
Shindano hilo pia lilihundhuriwa na Mrembo wa Tanzania ambae alikuwa ni Miss Dodoma, Miss Kanda ya Kati na ndiye anayeshikilia taji la Urembo wa Tanzania Kwa sasa Happiness Watimanywa. Pia Chief Judge alikuwa ni Father Hashim Lundenga ndiye aliyeongoza meza ya Majaji kumtoa mshindi huyo.









Mheshimiwa Sugu naye alikuwa akifuatilia kwa makini mashindano hayo.


Tazama picha zaidi katika mashindano hayo.....











Wawakilishi watatu walioiwakilisha Dodoma vizuri ambapo wawili walifika hatua ya tano bora na pia Mshiriki Namba 9 kufika hadi hatua ya tatu

Mshindi wa Pili Zena akionesha kipaji chake wakati wa talent na pia ndiye aliyepata zawadi ya Talent











Hashim Lundenga jaji  mkuu akitangaza matokeo


Happiness Watimanywa akimvalisha Crown mrembo wa Kanda ya Kati Dorice










Adelaida kushoto, Dorice katikatik (Mshindi) na Zena kulia wakiwa katika picha ya pamoja



Adelaida Mshindi wa Miss Dodoma yeye aliibuka mshindi wa tatu nae pia atawakilisha ngazi ya Taifa










Salama moja ya wadhamini wa mashindano hayo akiwa katika pozi na mshindi





Boss Ngasa nae alipata kidogo marashi ya Mshindi




 
Miss Tanzania Happiness Watimanywa akabidhi taji la Urembo wa Kanda ya Kati kwa Mshindi Mpya 2014. [Habari & Picha] Reviewed by Unknown on Saturday, June 21, 2014 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.