Top Ad unit 728 × 90

CBH FT. DULLyy SYKES - ABCD [Audio]

CBH Ft Dully Sykes – ABCD. CBH akiwa GERMANY aamua kuachia wimbo wake  akishirikiana na Prince Dully Sykes!!

                  
Msanii CBH akiwa nchini Ujerumani (Germany)  katika Tour yakimuziki itakayo isha mwishoni mwa mwezi wa 12 mwaka huu, atazunguka nchi mbali mbali za njee na mwisho kukutanishwa pamoja na mama yake mkubwa Tabia Mwanjelwa mwanamuziki nguli wakike wakimataifa alietamba sana na nyimbo zake kama Maisha ni Safari Ndefu akishirikiana na Makwizi Band, Jeni Mimi Ninahangaika na nyingine nyingi akiwa kama mwanamuziki wa kike wa kwanza kufanya muziki nakuwavutia wengi nchini Tanzania na Africa kiujumla kwa uzuri wa sauti yake, ujumbe katika tungo zake na utofauti mkubwa wa sauti yake yenyekuweza kufika code za juu sana nakuwashangaza watu wengi.
 
CBH  akiwa Germany toka mwezi wa 8 mwanzoni ameamua kuachia wimbo wake mpya akishirikiana na mkali wa muziki wa Bongo Flava Prince Dully Sykes aka Mr Misifa au Mtoto wa Kariakoo kama wengi wanavyo muita hivi sasa. Wimbo unaitwa ABCD, umerekodiwa G Records chini ya producer KGT Shadeed.
CBH amezumgumza kifupi juu ya wimbo huo akisema ni wimbo unaohusu kuvunja mahusiano na mtu unaempenda kwa sababu zakimabavu au kushinikizwa na watu wenye uwezo zaidi au nguvu. Ili kuweza kumuelewa zaidi amesema tusikilize wimbo huo akiwa na Dully Sykes. Amedai kumuheshimu sana Prince Dully Sykes kutokana na ushirikiano, upendo alio nao kwake kiujumla, CBH amemalizia nakusema Dully Sykes kwake ni kama kaka na anapenda sana moyo wake wakuwapenda wasanii wote. CBH akiongea amesema ‘’Dully Skykes ni msanii mwenye kujituma sana, na ninaheshimu sana kazi zake kama anavyozipenda kazi zangu. Dully anapenda sana wimbo wangu wa Am In Lovee’’
 
CBH ni msanii wa Tanzania alie anzisha style yake yakipekee ambayo iliwapelekea wasanii wengi waanze kuifanya nakuendelea kuifanya mpaka hivi sasa nakuubadilisha muzuki kwa kiasi kikubwa, huku watu wengi wakijaribu kuifananisha style hiyo na style ya muziki waki Nigeria. CBH alisimama nakuiita syle hiyo Sampa Music baada tu ya muziki wake kuanza kupigwa nchi nyingi za kiafrica nakuanza kupokea maswali mengi juu ya mtindo huo wa muziki anaofanya.
 
2008 – CBH Bestfriend.
Audio ilifanya studio za AM Records produced by Emanuelly Manecky na video ikafanyika mwaka 2010  baada ya miaka miwili ya wimbo huo kusumbua nchi mbali mbali za AFRICA na huku wengi wakijua CBH ni msanii toka Nigeria. Video ya Bestfriend imefanyika chini ya kampuni ya ShowBiz Defined edited by Eryne D. Epidu. Wimbo huu ukaingia katika top ten ya nyimbo bora zaki Africa ukikamata nafasi ya nne.
 
2011 – CBH Am In Lovee.
Wimbo wa pili wa CBH uliofanya vizuri sana katika vituo mbali mbali vya Television nje na ndani ya nchi. Na kuwafanya ma promota wengi toka nchi mbali mbali kuanza kumtafuta CBH kwaajili ya shows. Audio ya wimbo huu ilifanywa na producer wake aliefanya Bestfriend, Manecky katika studio za AM Records. Video ikafanyika mwaka 2011 mwishoni chini ya kampuni ya Visual Lab Next Lavel na Adam Juma anya vizuri
 
Zikafatia projects nyingi ikiwemo CBH ft B Skillz msanii toka Nigeria, wimbo Juliana. CBH akimshirikisha dada yake Witness Mwaijaga au Witnesz kama anavyojiita sasa, akiwemo na Ochu Eddy Sheggy mtoto wa marehemu Mzee Sheggy mwanamuziki mkubwa wa bendi zamani.Video ya wimbo huo imefanya na Adam Juma, Visual Lab Next Level katika mazingira yakinyumbani zaidi, wimbo unaitwa NADATA NAWEE.
 
CBH amesema hivi sasa anafanya project nyingi na wasanii mbali mbali wakimataifa huku akisubiri pia video yake mpya aliyofanya na BADI FILMS PRODUCTION from UGANDA directed by  LUKYAMUZI BASHIR. Audio by Andreey. UniversOl Rec.
CBH FT. DULLyy SYKES - ABCD [Audio] Reviewed by Unknown on Thursday, October 16, 2014 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.