Top Ad unit 728 × 90

GWANDA ZA KAMANDA RAS MAKUNJA HAZIFANANI NA ZA JESHI LA TANZANIA [Habari]

Gwanda za mkuu wa kikosi cha FFU-ughaibuni Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa band ambaye pia ni mmliki wa himaya ya Viumbe wa ajabu "Anunnaki Empire" yenye makao yake kule Ujerumani,gwanda za mkuu huyo hazina uhusiano wowote na JWTZ,na zoezi linaloendeshwa hapa bongo la kuwasaka wasanii wenye
mavazi ya kijeshi ,kamanda Ras Makunja na kikosi chake haliwahusu kwani wao wanaishi nje ya mipaka ya Tanzania,lakini kama ingekuwa wanaishi hapa labda ndio...


Habari zimetonya kuwa mwanamuziki huyo nyota wa kimataifa anayetamba na Bongo Dansi lake kule Ughaibuni Ras Makunja anakijua nini anachokifanya na pia anaheshimu sheria za nchi yake Tanzania kwani gwanda zake uzivalia nje ya mipaka ya Tanzania ,na anapokuja Tanzania kwa likizo yeye ni raia mwema tu vianzo vya habari vimetonya.mwanamuziki mwingine mwenye gwanda za kutisha katika kikosi cha Ngoma Africa band ni Soloist wa bendi hiyo Christian Bakotessa aka " Afande Chris-B Mshenzi wa solo gitaa" hawa jamaa wanatishaga kule ughaibuni majukwaani wao kuvaa gwanda ni kitu cha kawaida ulaya tena wakisindikizwa na ulinzi wa maaskari wa ulaya ! watupie jicho kambini kwao

GWANDA ZA KAMANDA RAS MAKUNJA HAZIFANANI NA ZA JESHI LA TANZANIA [Habari] Reviewed by Unknown on Saturday, October 25, 2014 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.