Mfahamu Producer aliyetamba miaka ya nyuma na hadi hivi sasa ngoma zake bado zinahit katika masikio ya wengi hapa bongo na nje ya bongo Mikka Mwamba
Miikka
Aleksanteri Kari
(amezaliwa tar. 16 Oktoba, 1971, mjini Helsinki,
Ufini)
ni mtayarishaji wa muziki na mhandisi wa sauti toka nchini Ufini-Tanzania.
Anafahamika zaidi kwa jina lake la kitayarishaji kama Miikka Mwamba.
Miikka Mwamba ni mtayarishaji mashuhuri sana kwa nchi ya Tanzania, na ameweza
kujibebea umaarufu mkubwa sana nchini Tanzania kunako miaka ya 2000.
Miikka
aliwahi kufanya kazi na wasanii mbalimbali wa nchini Tanzania. Wasanii hao ni: Dully Sykes, Inspector
Haroun, Lady Jay Dee, Mad Ice,
Chegge, Mandojo na Domo Kaya, Solid Ground Family, Complex, Zahrani (maarufu kama Big Punisher wa
Bongo), Only Face, Dknob na wengine wengi wa
kutoka Tanzania.
Miikka
Mwamba, ameshawahi kufanya kazi miaka mingi kwenye medani za muziki, filamu,
michezo ya kuigiza na dansi, ni swala ambalo si mara nyingi kufanyika kwa nchi
ya Ufini na Tanzania pia.
Miikka
alihitimu elimu yake ya msingi na secondary katika Lohja, ambacho ni chuo cha
sanaa (Torkkelin kuvataidelukio) alisomea Helsinki, na shahada ya uzamili (MA)
alipata Theatre Academy of Finland, Dept. of Light and Sound Design.
Nyimbo zilizotamba
- Julieta - Dully Sykes (2000)
- Athumani Mlevi - Solid Ground Family (2001)
- Baby Gal - Mad Ice (2002)
- Tupa Mawe - Zahrani na Complex (2001)
- Twenzetu - Chegge, Ferouz na Mh Temba (2005)
- Elimu Mitaani.com - Dknob (2003)
- Kitu Gani - Dknob (2007)
- Pia ndo producer aliyesaidia kuwaweka juu sana wasanii Mandojo na Domokaya.
Maelezo ya awaliJina la kuzaliwa: Miikka Aleksanteri KariAsili yake : FinlandAina ya muziki: Hip hip, R&B, Dansi & PopKazi yake: MtayarishajiTovuti: Mwambaproductions.com
Mfahamu Producer aliyetamba miaka ya nyuma na hadi hivi sasa ngoma zake bado zinahit katika masikio ya wengi hapa bongo na nje ya bongo Mikka Mwamba
Reviewed by Unknown
on
Wednesday, July 18, 2012
Rating:
No comments: