‘BABY MADAHA’ ADONDOKA GAFLA AKISHUTI FILAMU ALAZWA AMANA…!!
Msanii wa filamu ambaye pia anafanya muziki Baby Madaha, amendoka gafla wakati akishuti filamu yake mpya na kupoteza fahamu ambapo sasa amelazwa kwenye hosptali Amana jijini Dar es Salaam, na habari zinadai kuwa msanii huyo anasumbuliwa na ugonjwa wa kuanguka.
Chanzo cha habari ambacho kipo katika hosptali hiyo kilidai kuwa msanii
huyo kwa sasa huwezi kuzungumza kwani bado hali yake si nzuri na amepewa
muda wa kupumzika bila kufanya kazi yoyote akiwa chini ya usimamizi.
Hata hivyo kwa mujibu wa daktari ambaye anamtibu Madaha alitoa
taarifa kuwa msanii huyo wakati anapiga picha za filamu hiyo alikuwa
hajala chakula chochote badala yake alitumia kinywaji kikali kitu
ambacho kiliamsha tatizo lake lake.
Kwa mujibu wa madaktari wanadai kuwa ni kweli Madaha anasumbuliwa na
ugonjwa wa kuanguka lakini pia tatizo liilichangiwa na unywaji wa pombe
kali kabla hajala hivyo kwa sasa bado anafanyiwa vipomo ili kuona kama
kuna tatizo lingine.
Hata hivyochanzo cha habari hii kilipojaribu kufanya utaratibu wa kutaka kuzungumza naye walidai kuwa
hawezi kusema chochote kwani hata baadhi ya ndugu zake hawajapewa nafasi
ya kumuona ili kumpa muda zaidi wa kupumzika.
‘BABY MADAHA’ ADONDOKA GAFLA AKISHUTI FILAMU ALAZWA AMANA…!!
Reviewed by Unknown
on
Tuesday, September 11, 2012
Rating:
No comments: