DRE AONGOZA KWA UTAJJIRI WA HIP HOP CASH KINGS KWA 2012
Orodha ya kila mwaka ya Hip Hop Cash Kings kwa mwaka huu
ya jarida la Forbes jana imetoka na ina mfalme mpya. Si mwingine ni Andre Young
aka Dr. Dre.
Mwaka jana producer huyo ameingiza dola za kimarekani
milioni 110.
Hata hivyo pesa hizo hazijatokana na muziki bali ni
biashara yake inayolipa ya headphones zake za Beats by Dre. Kampuni ya Dr. Dre ilianzishwa mwaka 2008 na kumezewa
mate na kampuni ya utengezaji simu ya HTC iliyonunua asilimia 51 za hisa na
kuwekeza dola milioni 300.
Nafasi ya pili imekamatwa na Sean (Diddy) Combs
aliyeingiza dola milioni 45 mwaka jana ambazo nyingi zimetokana na hisa zake
kwenye kinywaji cha Ciroc vodka.
Jay-Z amekamata nafasi ya tatu kwa kuingiza dola milioni
38 mwaka jana kutoka kwenye muziki, hisa zake kwenye timu ya kikapu ya Nets,
kampuni ya vipodozi na hisa kwenye betri Duracell.
Kanye West amefuata katika nafasi ya nne kwa kuingiza
dola milioni 35 nyingi kutokana na mauzo ya albam yao ya pamoja na Jay-Z,
“Watch of Throne” na ziara ya albam hiyo duniani.
Nafasi ya tano imekamatwa na Lil Wayne ambaye albam yake
ya “The Carter IV” iliuza kopi kibao katika wiki ya kwanza na mwaka jana
aliingiza dola milioni 27.
Nicki Minaj amekuwa msanii pekee wa kike kuingia kwenye
list hiyo kwa kuingiza dola milioni 15 na kushika nafasi ya 8 nyuma ya Drake
aliyekamata nafasi ya 6 kwa kuingiza dola miliini 20.5 na mwanzilishi wa Cash
Money Records Bryan “Birdman” Williams katika nafasi ya 7 aliyeingia dola milioni
20.
Eminem amejikongoja pia kwa kuingiza dola milioni 15 na
kushika nafasi ya 9 huku nafasi ya 10 ikishikwa na Ludacris aliyeingiza dola
milioni 12.
DRE AONGOZA KWA UTAJJIRI WA HIP HOP CASH KINGS KWA 2012
Reviewed by Unknown
on
Thursday, September 06, 2012
Rating:
No comments: