Jini Kabula na Jack Pentzel wakanusha kuwa na uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja
Kwa muda mrefu waigizaji wa kike wa Bongo Movies, Jack
Pentzel na Miriam Jolwa aka Jini Kabula wamekuwa wakisakamwa na skendo ya
usagaji kutokana na picha iliyosambaa
kwenye mtandao inayowaonesha wakibusiana.
Hata hivyo wote wameendelea
kukanusha kutojihusisha na vitendo hivyo kwa kudai kuwa walikuwa kazini.
Akiongena na kipindi cha Tagz Weekly cha DTV, Jack amesema
hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Miriam kwakuwa zile ni picha
zilizochukuliwa wakati wakishoot movie.
“Mi mwenyewe nimezisikia kama wewe ulivyozisikia, lakini
ukweli ni kwamba mimi ni msanii, ni msanii wa filamu nafanya kazi za kuelimisha
jamii, kwamba jamii ntaifundisha kwamba ifanye hivi ntaikosoa ifanye hivi.
Kwahiyo zile ni picha ambazo zilipigwa wakati tupo location, na sio kwamba zile
picha walizoziona wao ndio kile kitu sisi tulichokuwa tunakifanya. Sisi
tulikuwa tunaigiza, hakuna uhalisia wowote wa kitu tulichokuwa tunakifanya”,
alisema.
“Mimi nina mtu wangu, mimi nina mpenzi wangu, kwanza siwezi
kuwa na mahusiano na mwanamke mwenzangu, kwasababu atanifanya nini mpaka mimi
niridhike?”
Kwa upande wake Miriam, naye alikanusha kuwa na uhusiano na
mwanamke mwenzake na kusisitiza kile alichokisema mwenzie.
“Ni kweli hizo picha zipo, lakini
sio kama namaanisha mimi na Jack Pentzel tulikuwa tunafanya huo uchafu. Hiyo ni
movie tulikuwa tunacheza, mimi nilikuwa kama namuapproach Jack, yaani mimi ndio
yule mwanamke msagaji halafu yeye ndio demu wangu. Na hiyo movie sijui kwanini
inachelewa kutoka,” alisisitiza Miriam.
Picha hii ndo iliyoleta utata kwa watu wengi |
Jini Kabula na Jack Pentzel wakanusha kuwa na uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja
Reviewed by Unknown
on
Monday, September 10, 2012
Rating:
No comments: