Mwasiti agongewa ngoma na MMAREKANI!
Zamani wengi tulikuwa tukimwona kama binti mdogo, lakini hivi sasa
naweza kusema ni mdada mkubwa haswaa, huyu si mwingine bali ni Mwasiti
Almasi ambae kwa sasa anafanya vizuri sana na pini lake MAPITO.
Akiongea kwa njia (SMS) wikiendi iliyoisha, mdada huyu ambaye ni zao
la nyumba ya vipaji ya (THT) ameweka wazi kuwa amefanya ngoma na
producer mkubwa marekani anaeitwa Hakeem.
Kwa taarifa yenu tu ni kwamba Hakeem ameshawahi kufanya ngoma na
wakali kibao duniani akiwemo Akon kwenye pini (i wanna be with
you),ameshafanya na Youssu ndor na wakali wengine kibao.
"Nimefanya nae ngoma mbili moja ikizungumzia wanawake na matatizo
yanayowakuta, ila ya pili ipo kibongo fleva zaidi, nimefurahi sana na
naiheshimu sana kazi yangu."
Mwasiti agongewa ngoma na MMAREKANI!
Reviewed by Unknown
on
Monday, September 10, 2012
Rating:
No comments: