Tamasha la kitamaduni la Mwafrika mlangoni
Kwani tamasha hilo limeandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya
Team Jambo, ambayo imeshapokea washiriki kutoka nchini Nigeria, Afrika
Kusini, Kenya na Canada wakiomba kushiriki kwenye tamasha hilo kama
watazamaji.
Si lingine bali ni lile Tamasha la Sanaa na Utamaduni wa Mwafrika,
litakalohusisha vyakula vya asili na limeandaliwa kwa lengo la kukuza na
kuenzi Utamaduni wa Mwafrika.
Nay Mwneyekiti wa Team Jambo, Augustin Namfua, alisema kwamna
wameshakamilisha taratibu zote za kufanikisha tamasha hilo ambalo ni
muhimu sana kwa wale wanaojishughulisha na shughuli za sanaa zikiwemo za
Kitamaduni zaidi.
Mbali na hilo tamsha hilo litrakuwa ni la siku tisa, na kutakuwa na
matukio sita muhimu ambayo yatahusika kulipamba, ikiwemo upatikanaji wa
vyakula vya asili, shughuli za ngoma za asili na mdahalo wa wasanii
ukiwahusisha wachongaji, wachoraji na wanamuziki.
“Lakini pia, katika siku za tamasha hilo kubwa kufanyika kwa wana
sanaa na utamaduni hapa nchini, kutakuwa na siku moja ya matembezi,
ambapo washiriki watakuwa wamevaa mavazi ya asili na kupita mitaa muhimu
jijini Arusha,” alisema.
Alitoa wito kwa wasanii wa uchoraji, uchongaji na wajasiriamali
wengine waliopo katika sekta hiyo ya sanaa, kujitokeza kujiandikisha
kushiriki tamasha hilo ambalo ni muhimu kwao.
Tamasha hilo litawika ndani ya viwanja vya wazi vya mzunguko wa
Kijenge na baadhi ya shughuli zitafanyika katika Hoteli ya Naura Spring
na Via Via, katika siku maalumu ikiwemo ngoma za asili.
Tamasha la kitamaduni la Mwafrika mlangoni
Reviewed by Unknown
on
Saturday, September 08, 2012
Rating:
No comments: