Hii Ndio Idadi ya Mashtaka Yanayo Mkabili Lord Eyez Baada ya Kuiba Vitu vya Gari ya Ommy Dimpoz
Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi wa
Kinondoni Charles Kenyela amethibitisha jeshi lake kumshikilia msanii
Lord Eyes ambae toka weekend iliyopita taarifa zake zimesambaa baada ya
kushutumiwa kuhusika na wizi wa vifaa mbalimbali kwenye gari la mwimbaji
Ommy Dimpoz.
Namkariri Charles Kenyela akisema “ni kweli Isaac
Waziri Maputo mwenye umri wa miaka 28 alikamatwa tarehe 20 mwezi wa kumi
usiku maeneo ya Kinondoni, kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu ni kutokana na
taarifa tulizozipata kupitia kwa binti mmoja aitwae Kurushinde Hillary
(22) mwenye asili ya kiburushi lakini mkazi wa Mwananyamala kwa Makoma
Dar es salaam, alikamatwa siku hiyo hiyo kabla ya Lord Eyes”
“Alikamatwa
kuhusiana na matukio ya wizi kwenye magari yani kuna mtindo ambao
umeibuka ambapo ukipaki gari yako gari nyingine ya wezi inakuja inapaki
jirani na gari yako ambapo kwa muda mfupi wanafanya utundu wao
wanaoujua, wanafungua gari na kuiba mali iliyoko ndani, mara baada ya
huyu binti kukamatwa katika kuhojiwa mtandao wake anaoshirikiana nao
alimtaja mtuhumiwa Isaac Waziri Maputo (Lord Eyes)” – Kamanda Kenyela
Kwenye
sentensi nyingine Kamanda Kenyela amesema “watu wengi wamelalamika
kuibiwa laptop zao, mabegi, mifuko na hata silaha kwa maana mtu anakua
anajiamini anaacha kwenye gari akiamini kwamba ameshalock lakini watu
hawa na mtandao wao wamekua ni hatari kiasi kwamba wameliza watu wengi”
“Watuhumiwa
hawa wawili Kurushinde na Lord Eyes tunawashikilia kwa tuhuma zipatazo
30, yani matukio mbalimbali 30 pengine yanaweza yakaongezeka ambayo
yameripotiwa kutokea katika maeneo mbalimbali kama vile Mlimani City,
Kijitonyama, ufukwe wa bahari kama Coco beach, kwenye kumbi mbalimbali
za starehe na pia kwenye maeneo ambayo kunakua na harusi, sehemu ambazo
kunakua na magari mengi watu hawa ndio huwa wanaitumia hiyo nafasi
kufanya uhalifu, tunawashikilia kwa makosa ya wizi”
Hii Ndio Idadi ya Mashtaka Yanayo Mkabili Lord Eyez Baada ya Kuiba Vitu vya Gari ya Ommy Dimpoz
Reviewed by Unknown
on
Thursday, October 25, 2012
Rating:
No comments: