Albam ya Rihanna ‘Unapologetic’ yakamata nafasi ya kwanza kwenye chart za Billboard
Rihanna amefanikiwa kuiingiza moja kwa moja albam yake mpya Unapologetic kwenye chart za albam 200 za Billboard.
“Unapologetic,” iliyokamata nafasi ya kwanza pia kwenye iTunes
katika nchi 43 ikiwa masaa tu tangu itoke November19, iliuza kopi
238,000 kwa mujibu wa Billboard.
Wimbo wa kwanza kutoka kwenye albam hiyo, “Diamonds” upo kwenye top
five ya Billboard Hot 100 wiki iliyopita na kuwa single ya 12 ya Rihanna
kuwahi kukamata nafasi ya kwanza.
Albam hiyo imefanyiwa promotion ya uhakika na Rihanna aliyefanya
ziara ya siku saba kwenye majiji saba duniani kote kwa kusafiri na
waandishi wa habari pamoja na mashabiki wake.
Albam ya Rihanna ‘Unapologetic’ yakamata nafasi ya kwanza kwenye chart za Billboard
Reviewed by Unknown
on
Wednesday, November 28, 2012
Rating:
No comments: