Lord Eyes Kutengeneza Track Mpya Kwa P-Funk Majani
Msanii Lord Eyes ambae anatokea kwenye kundi la HipHop hapa Tanzania almaarufu kama Weusi Linalo waunganisha wasanii kama Joe Makini, Nicki wa Pilli, G-nako na wengine. Sasa habari kutoka kwa msanii huyo baada ya kukaa rumande kwa wiki chache kidogo kutokana na kesi inayomkabili, Lord Eyes ameamua kurekodi track yake mpya akiwa amemshirikisha Damian Mihayo, ila masanii huyo hakuwa tayari kusema jina la track hiyo bali alisema anataka kuifanya iwe surprise kwa mashabiki wake. Track hiyo inafanyika chini ya usimamizi wa P-Funk Majani katika Studio za Bongo Records ambapo Producer huyo alipost kwenye ukurasa wake wa Facebook hapo jana.
Lord Eyes Kutengeneza Track Mpya Kwa P-Funk Majani
Reviewed by Unknown
on
Friday, November 23, 2012
Rating:
No comments: