SHOW YA SPACK DODOMA YASHINDWA KUFANYIKA
Ile show iliyotarajiwa kufanywa na Msanii Spack mjini Dodoma haipo tena kutokana na Spack kudai maslahi ya show hiyo hayakuwa ya kuridhisha tofauti na alivotarajia.
Tuliongea na mdhamini wa Show hiyo ambaye ni Boss Ngasa chini ya G & G Internet Cafe naye alikiri kwamba ni kweli show hiyo haipo tena baada ya spack kuikacha.
Lakini habari zaidi zinadai kwamba Spack alipata show nyingine Zanzibar yenye mkwanja mrefu zaidi kitu kilichomfanya aikache ya Dodoma na kwenda Zanzibar ambako alipiga show na baadae kuelekea Mwanza tena kwa Show nyingine ambayo nayo ilishafanyika.
Vile vile Spack mwenyewe anadaii kwamba ile ngoma yake ya 'Tangu nitoke Jela' anaiandalia Muvi ambayo itaendana na maudhui yaliyopo katika songi hilo, so mashabiki wakae mkao wa kuipokea Muvi hiyo ambayo mhusika mkuu ni yeye mwenyewe Spack..
SHOW YA SPACK DODOMA YASHINDWA KUFANYIKA
Reviewed by Unknown
on
Monday, November 26, 2012
Rating:
No comments: