TAARIFA KUHUSU UGOMVI WA JAY Z NA MWIGIZAJI ROBERT DE NIRO.
Inasemekana siku chache zilizo pita Mwigizaji Mkubwa na Mkongwe Duniani Robert De Niro alitaka kufanya mazungumzo na Rapper Jayz kuhusu kazi tofauti alizo taka kufanya nae mjini New York. Robert alimpigia simu Jay z mara sita na kumuachia ujumbe akipata nafasi ampigie simu.
Jay z hakufanya hivyo mpaka walivyo kuja kukutana juzi kwenye moja ya party kubwa New York na Ndio hapo Robert alipo mbwatukia Jay z mbele za watu kuhusu kukosa nidhamu na kujifanya yeye ndio yeye au mjanja sana kuliko wakubwa zake .
Jay z na Mke wake Beyonce walijaribu kumtuliza Robert kwani alikuwa akutumia sauti ya juu sana lakini ilishindikana. Jay z alijiskia aibu sana na kumuomba msamaha Robert hapo hapo.
TAARIFA KUHUSU UGOMVI WA JAY Z NA MWIGIZAJI ROBERT DE NIRO.
Reviewed by Unknown
on
Monday, November 19, 2012
Rating:
No comments: