Baadaya kujichora tatoo yenye jina la Prof Jay na kupost picha yake akionesha tatoo hiyo katika mitandao ya kijamii Twitter na Facebook na hatimae mashabiki wake kuwa na maswali mengi juu ya tatoo hiyo Dj CHOKA ameamua kuweka wazi ni kwa nini ameamua kuchora tatoo hiyo..
"NDUGU
ZANGU NIMESOMA COMMENTS ZENU NA NIKAWAELEWA SANA SIWEZI PINGA MAWAZO YA
WATU OK. Sasa ni hivi nia na dhumuni la kuchora tattoo yenye jina la
PROF JAY ni kwamba nusu ya maisha yangu yote mpaka kufika hapa nakuwa na
familia yangu yeye ndio nguzo yangu imara na nuru ya ushauri wangu kila
siku iendayo kwa mungu. Na kama mlikuwa hamjui me sio shabiki wa PROF
JAY mimi ni ndugu na nimdogo ambaye wazazi wangu waliponiruhusu kulelewa
na Prof Jay ndio nikaanza kufundishwa huu mziki wa bongo mpaka sasa
nimekuwa na kusimama mwenyewe. So tattoo hii ni heshima ambayo
haitofutila milele mpaka nakufa na why umsifie mtu akisha kufa? Nampa
heshima yake akiwa hai ili ajue kwamba huu wino unamaana nyingi sana.
Natukuza vya nyumbani vya nje sivijui kiundani...ASANTENI"
Hayo ndo yaliyosemwa na DJ CHOKA katika ukurasa wake wa FACEBOOK..
No comments: