Ben Pol azungumzia vipaji vya wasanii wa Bongo na Ugumu wa Game la Muziki Bongo
Ben Pol ambaye ni moja ya wasanii wanaotamba sana katika game la muziki wa Bongo amezungumza ya kwake anayoyaona kuhusiana na vipaji na uwezo mkuubwa walio nao wasanii wa Bongo kwa kusema kwamba.."wasanii wa Tanzania wana uwezo mkubwa sana hasa katika ufanyaji wa kazi zao za muziki kwa ujumla manake wanafanya mambo mengi wakiwa peke yao, tofauti na wasanii wenzetu wa nchi za Ulaya ambao wanakuwa wakiyafanya mambo yao chini ya usimamizi wa timu fulani ambaoyo ni kuanzia kutunga mashairi, uhakiki wa sauti, usimamizi wa mambo ya masoko na mambo mengine mengi yanayomhusu msanii mmoja'...
Pia pamoja na hayo aliweza kueleza pia ugumu wa Muziki hapa Tanzania kwa kusema wasanii bado hawajafika malengo zaidi ni kwamba wanafaidika kidogo sana tofauti na malengo halisi wanayokuwa wamejiwekea, pia kuna baadhi ya wasanii wanaoridhika mapema wakati walichokipata unakuta bado hakifanyi lolote katika maisha yake...
Msikilize hapa chini akiyazungumza hayo katika EVENT PAGE ya Fleva GX (Impact Fm)..
Ben Pol azungumzia vipaji vya wasanii wa Bongo na Ugumu wa Game la Muziki Bongo
Reviewed by Unknown
on
Monday, March 11, 2013
Rating:
No comments: