Mashindano ya kumtafuta mrembo wa Kanda ya kati yamefanyika usiku wa kuamkia leo tar. 21.06.2014 katika ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma ambapo mshindi wa mashindano hayo yaliyoshirikisha warembo kadhaa toka mikoa mitatu ya Dodoma, Singida na Tabora amepatikana.
Kinyang'anyiro hicho kilileta ushindani mkubwa hasa ukizingatia kwamba washiriki toka mikoa yote walijipanga vya kutosha na kikubwa wote walikuwa ni washindi walioiwakilisha mikoa yao.
Mrembo Dorice Molel toka Singida ndiye aliyenyakuwa taji hilo akifuatiwa na mshindi wa pili 'Zena' toka Tabora na wa tatu 'Adelaida' toka mkoani Dodoma.
|
Meza Kuu ya Majaji |
|
Wazazi wake na Miss Tanzania Happiness Watimanywa nao walikuwepo kushuhudia kinyang'anyiro hicho |
|
Naibu waziri wa Michezo, Vijana, Habari na Utamaduni Juma Nkamia akifungua mashindano hayo |
Washindi hawa watatu ndio watakaowakilisha Kanda ya Kati katika mashindano ya urembo ngazi ya Taifa yaani Miss Tanzania 2014/2015.
Shindano hilo pia lilihundhuriwa na Mrembo wa Tanzania ambae alikuwa ni Miss Dodoma, Miss Kanda ya Kati na ndiye anayeshikilia taji la Urembo wa Tanzania Kwa sasa Happiness Watimanywa. Pia Chief Judge alikuwa ni Father Hashim Lundenga ndiye aliyeongoza meza ya Majaji kumtoa mshindi huyo.
|
Mheshimiwa Sugu naye alikuwa akifuatilia kwa makini mashindano hayo. |
Tazama picha zaidi katika mashindano hayo.....
|
Wawakilishi watatu walioiwakilisha Dodoma vizuri ambapo wawili walifika hatua ya tano bora na pia Mshiriki Namba 9 kufika hadi hatua ya tatu |
|
Mshindi wa Pili Zena akionesha kipaji chake wakati wa talent na pia ndiye aliyepata zawadi ya Talent |
|
Hashim Lundenga jaji mkuu akitangaza matokeo |
|
Happiness Watimanywa akimvalisha Crown mrembo wa Kanda ya Kati Dorice |
|
Adelaida kushoto, Dorice katikatik (Mshindi) na Zena kulia wakiwa katika picha ya pamoja |
|
Adelaida Mshindi wa Miss Dodoma yeye aliibuka mshindi wa tatu nae pia atawakilisha ngazi ya Taifa |
|
Salama moja ya wadhamini wa mashindano hayo akiwa katika pozi na mshindi |
|
Boss Ngasa nae alipata kidogo marashi ya Mshindi |
No comments: