Top Ad unit 728 × 90

Mr Nice kuja kimduara zaidi

Alisema kwamba amefurahishwa kuona kwamba mashabiki wake kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi, wanaendelea kumpa sapoti ya ajabu pindi aliporejea tena kwenye gurudumu la muziki baada ya kumwa kimya kwa kipindi cha miaka kadhaa.
Si mwingine bali ni yule Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini, Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’ amesema baada ya kupokea maombi mengi ya mashabiki, ameamua kuanza kuwatendea haki wakazi wa Kanda ya Ziwa baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kwani hakutegemea kupata mapokezi makubwa kwa kiasi hicho, wakati akiandaa na ufyatuaji wa albamu yake ya 'Tabia gani?' aliyoikamilisha siku za usoni.
Alisema albamu hiyo itakwenye kwenye mahadhi ya mduara, huku ikionekana kufanya vyema kwenye vituo vya radio na hata vya televisheni mbalimbali hapa nchini.
Mbali na hilo alisema kwamba amefurahishwa kwa kuona wimbo wake mwingine uitwao 'Mfalme', aliowashirikisha wanamuziki kutoka Mexico na Hispania ukikubalika.

Chanzo DarHotWire
Mr Nice kuja kimduara zaidi Reviewed by Unknown on Thursday, July 19, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.