Top Ad unit 728 × 90

ANOLD AFURAHIA KURUDI UPYA KATIKA MUVI


Anold Schwarzenegger amesema amejishangaa mwenyewe baada ya kujikuta akirudi tena kwenye uigizaji wa filamu. Gavana huyo wa zamani wa jimbo la Califonia alidhani asingerudi tena kwenye uigizaji wa filamu baada ya kujihusisha na siasa lakini alishangaa jinsi alivyofurahia kuhusika kwenye filamu za 'The Xpendable' I & II.

Aliuambia mtandao mmoja kwamba "Nilipokuwa Gavana nilikuwa nikitembelea maeneo yanapofanyika filamu na kuwashukuru watu kufanyia jimboni California kwa sababu ni kitu kizuri kwa uchumi wa jimbo langu"

Amesema kuwa siku moja Tom Cruise alikuwa akifanya Film na alikuwa amening'inia miguu juu kwenye scene ya mapigano (action) na nikawa nasema "Nina furaha mimi sining'inii tena kwenye filamu za Action kama ile" Lakini mkongwe huyo amejikuta akirufahia upya tena baada ya kushiriki Muvi hiyo na kusema kwamba anafurahi sana kufanya muvi za action kwa mara nyingine na vile vile amefurahi kuigiza na wasanii wenzie wakongwe kama Bruce Willis, Sylvester Stallone, Jean Claude 'Van Damme na wengine wengi katika Muvi hiyo ya The xpendable II.
ANOLD AFURAHIA KURUDI UPYA KATIKA MUVI Reviewed by Unknown on Wednesday, August 15, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.