Top Ad unit 728 × 90

Linex, Suma Lee & Baba Levo wapata ajali!

Taarifa iliyotufikia toka kwa msanii Linex ni kwamba akiwa na wasanii wenzake Baba Levo na Suma Lee wamepata ajali wakielekea mkoani Kigoma kikazi.

Kwa mujibu wa Linex, wakiwa wanaelekea kigoma ambapo watakuwa na show wikiendi hii..walikutana na ajali hiyo lakini kwasababu hawakuwa na mwendo kasi waliweza kusalimika.
Dancer mmoja wa Suma lee ameumia Mguu na Gari la Suma Lee ndio lililoumia sana upande wa mbele,kwani taa zimepasuka na sehemu ya mbele kuharibika sana.

Ajali ilisababishwa na basi la abiria lililokuwa katikati ya barabara kwenye kona kali, ambapo ili kulikwepa lazima Suma angetakiwa atoke nje ya barabara, ndipo gari ilipomshinda na kugonga mti.
Linex ,Baba levo na Suma lee wana show tatu weekend hii Ijumaa mjini Kigoma ,

Jumamosi ni Kasulu na Jumapili ni Bujumbura.
Linex, Suma Lee & Baba Levo wapata ajali! Reviewed by Unknown on Wednesday, August 29, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.