Top Ad unit 728 × 90

MAISHA PLUS YAJA SOON….MSHINDI WA MWAKA HUU KUONDOKA KITITA CHA TSH MIL. 20…!!


Maisha Plus is back na shughuli ya kusaka washiriki wa kuingia kijijini mwezi October utaanza rasmi siku ya Jumatatu ijayo. Tofauti na usaili wa mashindano yaliyopita, vijana hao 26 watatafutwa katika vijiji ambavyo Mama Shujaa wa chakula wapatao 15 walipatikana kutokana na mchakato uliofanywa na shirika la chakula na kilimo la Uingereza la Oxfam ambalo msimu huu litashirikiana na waratibu wa shindano hilo.

“Vijana wa Maisha Plus wataingia kijijini, watakwenda kuchanganyika na hao kinamama, watakaa kwa siku tatu jumla kwa maana ya kwamba watakaa siku 12, 13 na siku 14. Katika hizi siku tatu vijana watakapochanganyika na hawa akinamama mle ndani tutatengeneza makundi ambapo kila mama mmoja mzalishaji wa chakula atakuwa na timu ya vijana tuseme watatu, wanne, sita kulingana na idadi ya washiriki wa Maisha Plus ambayo mwaka huu imeongezeka kutoka 18 hadi 26“-
Kipanya.

Kwa mujibu wa
Masoud Kipanya ambaye ndiye mratibu wa shindano hilo, mshindi wa mwaka huu atajinyakulia kitika cha shilingi milioni 20. [source: DarTalk]
MAISHA PLUS YAJA SOON….MSHINDI WA MWAKA HUU KUONDOKA KITITA CHA TSH MIL. 20…!! Reviewed by Unknown on Friday, August 24, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.