Top Ad unit 728 × 90

SINTA IS BACK KWENYE GAME LA MUVI AJA NA "THE RETURN OF J.LO"

Hii ndo Picha ya Cover ya Muvi hiyo

Pamoja na kuamua kurudi kwake ktk Game lal Muvi Msanii asiyeishiwa vituko Bongo ambaye alipotea kwa muda mrefu na kuonekana tena siku za karibuni ameamua kuja upya kwa kishindo kwa kuibuka na Muvi yakek mwenyewe aliyoipa jina na "The Return of J.Lo" Japo wadau nchini wamehoji na kujiuliza ni jinsi gani kaweza kutumia jina la mtu ama msanii huyo wa Nje bila makubaliano yoyote yale?

WADAU wengi wa tasnia ya filamu bongo wameanza kuingiwa na shaka kubwa, baada ya msanii wa filamu Christine John ‘Sintah’, kutumia jina la msanii wa Marekani Jennifer Lopez aka JLO, kwenye filamu yake na kazi hiyo.

Mazungumzo yaliyofanyika na wadau kadhaa wa tasnia hiyo na wote walionekana kuwa na mawazo tofauti kuwa wanshindwa kuelewa ni kitu gani kilimfanya hadi mwanadada huyo kutumia jina mtu bila idhini yake.


Mwandishi alimtafuta ‘Sintah’, ili aweze kuwajibu wadau hao, katika kujibu kwake alidai kuwa ameamua kutumia jina hilo kwani huo ndiyo wakati wake yenye kwani anakuja kwa kishindo kikubwa katika tasnia cha filamu hivyo mashabiki wake waondoe shaka juu ya hilo.


Hata hivyo aliongeza kuwa sababu kutumia jina hilo kingine ni kwamba anampenda sana mwanadada huyo na haoni kama inaweza kuleta matatizo ingawa ni kweli hakuzugumza naye juu ya hilo.


“Ni kweli kwa msanii mwigine anaweza kunishtaki kwani nimetumia jina lake pasipo mwenyewe kujua, lakini nachowaomba watanzania wajue kila kitu kipo sawa na kazi yangu imetulia hivyo waitazame kwa umakini ili wajue kitu gani kinachozungumzwa,”
alisema.


SINTA IS BACK KWENYE GAME LA MUVI AJA NA "THE RETURN OF J.LO" Reviewed by Unknown on Friday, August 24, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.