Top Ad unit 728 × 90

Sijafukuzwa bali Nimejiondoa - Suma

Siku chache baada ya mkurugenzi wa kampuni ya MTANASHATI, maarufu kwa jina la Ostaz Juma na Musoma kutangaza kuwatimua  ndani ya kampuni yake msanii Suma Mnazaleti na aliyekuwa meneja wa wasanii aliyefahamika kwa jina la Maneno, kisa akikitaja kuwa ni utovu wa nidhamu, Suma Mnazaleti ameibuka na kusema kuwa hakufukuzwa bali yeye ameamua kujiondoa mwenyewe.
Akinukuliwa kwa mdomo wake Suma Mnazareti, alisema..."Nimeamua kujitoa mtanashati, na sababu kubwa katika zote ya kujitoa ni kwamba nilifwata kazi kwa Ostaz na sio hela zake, so nilichokuwa nadhania ntakipata mtanashati hakipo,Boss anatafta zaidi sifa na ustaa Tanzania na mimi mziki ni kazi yangu.
Ostaz anaweza akagawa mamilioni kwa watu ili atajwe lakini anashindwa kulipa hela ya maana kwa ajili ya video, matokeo yake anatoa shilingi laki tatu? unadhani tutaweza kushindana na video kama za kina Ay za million 30?. nimeuza mpaka balackberry yangu kuongeza kwenye pesa za kukamilisha video yangu, wakati hata nilivyokua nahustle mwenyewe sikuwahi kuuza simu yangu.
so nimejiondoa maana sioni faida yoyote, na mimi mziki kwangu ni masha nataka nifike mbele zaidi.
Kampuni ya Mtanashati inawamanage wasanii wazuri wengi tu kati yao ni kama Dogo janja, Amazon na PNC.
Sijafukuzwa bali Nimejiondoa - Suma Reviewed by Unknown on Tuesday, August 28, 2012 Rating: 5

No comments:

All Rights Reserved by Dj Mchomo © 2014 - 2015
Powered By WordPress24x7

Contact Form

Name

Email *

Message *

Dj Mchomo. Powered by Blogger.